Black Butterfly
Senior Member
- Aug 31, 2022
- 130
- 368
Ziara ya Waziri wa Nishati, January Makamba nchini Indonesia imemalizika kwa kuimarisha ushirikiano wa nchi hizo mbili katika sekta ya umeme, mafuta na gesi.
Makamba kwa nyakati tofauti alikutana na Waziri wa Nchi anayeratibu biashara zinazomilikiwa na Serikali, Luhut Pandiaitan, Waziri wa Nishati na Rasilimali za Madini Mhe. Arifin Tasrif, Mwenyekiti wa Jukwaa la Biashara na Viwanda, Bw. Suryo Sulisto, Rais wa Shirika la Umeme la Indonesia (PLN), Bw. Darmawan Prasodjo, Makamu wa Rais wa Kampuni ya Mafuta ya Taifa ya Indonesia – Pertamina, Bw. Salyadi Sapurta, na Rais wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya MEDCO, Bw. Hilmi Panigoro.
Waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Indonesia, Macocha Tembele, Kamishna na Petroli na Gesi, Bw. Michael Mjinja, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la TPDC Dr. James Mataragio na maafisa kutoka TANESCO na PURA.
Waziri Makamba amesema, “Tanzania inahitaji kuimarisha uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa Nishati ya Umeme kwa wananchi wake na hivyo Indonesia ni nchi ambayo imepiga hatua kubwa na kwa haraka katika kufanikiwa kuwafikishia wananchi wake huduma hiyo. Hatuna budi kujifunza kutoka kwenu.”.
Hadi sasa Indonesia imeshafanikiwa kufikisha huduma ya Umeme kwa asilimia 99.9 ya wananchi wake licha ya nchi hiyo kuwa na visiwa zaidi ya 1000.
Ikumbukwe kwamba Pertamina na kampuni yake tanzu ya Maurel and Prom zinafanya kazi Tanzania katika kitalu cha Mnazibay kwa kazi zote zinazoendelea.
“Serikali inatambua kitalu hicho bado kina rasilimali ya gesi nyingi zaidi ardhini, lakini uwekezaji wake hauridhishi. Serikali ya Tanzania inategemea sana uzalishaji wa gesi kutoka Mnazibay, ni vema Pertamina ikaliangalia jambo hili kwa kina kwa kushrikiana na mbia wake TPDC.” - Waziri Makamba.
Baada ya Kikao hicho Viongozi hao wa nchi mbili walikubaliana mambo yafuatayo; kusaini makubaliano ya awali ya ushirikiano kati ya Wizara na Nishati ya Tanzania na Wizara ya Nishati na Rasilimali za Madini ya nchini Indonesia katika kuendeleza miradi ya jotoardhi, usafirishaji wa umeme, utafutaji wa mafuta na gesi asilia na mafunzo ya kuongeza uwezo kwa wataalamu.