Tanzania yasaini Mkataba wa Ujenzi wa Reli ya SGR (Kigoma - Burundi) kwa Tsh. Trilioni 5.6

Mtoa Taarifa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2024
Posts
213
Reaction score
671
Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC) na nchi ya Burundi leo Januari 29, 2025 zimesaini mkataba wa ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR yenye urefu wa kilomita 282 kutoka Uvinza mkoani Kigoma hadi Musongati nchini Burundi.

Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa kwa upande wa Tanzania na Waziri wa Miundombinu wa Burundi, Kapteni Dieudonne Dukundane, wamesaini mkataba huo jijini Dar es Salaam ambao utagharimu shilingi Trilioni 5.6.

Ujenzi wa reli hiyo ya kisasa unatarajiwa kuwa kichocheo kikubwa cha shughuli za kiuchumi na kijamii baina ya nchi zote mbili.
 
Burundi wamechangia kiasi gani kwenye hyo trioni 5.6? Hv bajeti ya Burundi kwa mwaka mmoja inafika ata trioni 5 kweli?
 
Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC) na nchi ya Burundi leo Januari 29, 2025 zimesaini mkataba wa ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR yenye urefu wa kilomita 282 kutoka Uvinza mkoani Kigoma hadi Musongati nchini Burundi.

Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kadogosa kwa upande wa Tanzania na Waziri wa Miundombinu wa Burundi, Kapteni Dieudonne Dukundane, wamesaini mkataba huo jijini Dar es Salaam ambao utagharimu shilingi Trilioni 5.6.

Ujenzi wa reli hiyo ya kisasa unatarajiwa kuwa kichocheo kikubwa cha shughuli za kiuchumi na kijamii baina ya nchi zote mbili.
Muendelezo wa kazi njema ya Dr Samia .

Anaanzia alipoishia kusonga mbele 👇👇

View: https://www.instagram.com/p/DFaXHoKNdB-/?igsh=YmZnZGIwOWw3am9p
 
Kama lengo ni kongo sawa lakini kama lengo ni burundi hizo pesa wamezitupa chooni na ukitegemea burundi muda wowote "wanakinusha"
 
Back
Top Bottom