Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Gerald Kusaya amesema Tanzania haina mpango wa kuanza kuruhusu kilimo cha bangi na badala yake amewataka wananchi kujikita katika kilimo cha mazao mengine yenye tija.
Kamishna Jenerali Kusaya ameyasema hayo jijini Dodoma katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupambana na dawa za kulevya yatakayofanyika kitaifa jijini Dodoma Juni 26 mwaka huu yakiwa yamebeba kauli mbiu ya tuelimishane juu ya tatizo la dawa za kulevya kuokoa maisha.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Dodoma Bw.Antony Mtaka amesema mkoa umejipanga katika kushiriki maadhimisho hayo kitaifa ambapo amezungumzia mpango wa mkoa huo katika kupambana na kilimo cha bangi.
Chanzo: ITV