Leo March 16, 2018 Jarida maarufu la Business Chief limeitaja Tanzania kama taifa la pili lenye uchumi unaokuwa kwa kasi zaidi barani Africa. Tanzania uchumi wake unakua kwa asilimia 7 imeshika nafasi ya pili nyuma ya Ivory Cost ambayo uchumi wake unakuwa kwa asilimia 8.5.
Orodha hiyo inayotangazwa kila mwaka, imesheheni mataifa ya Africa mashariki kwani ndio ukanda ambao umetajwa kuwa na uchumi unaokuwa kwa kasi, huku kilimo, utalii, usafiri, mawasiliano na biashara zikitajwa kama sekta zinazotazamwa na kuingiza vipato vikubwa
Source : MillardAyo