Tanzania yashiriki katika maonesho ya kimataifa ya paris 2020, Ufaransa

Tanzania yashiriki katika maonesho ya kimataifa ya paris 2020, Ufaransa

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
February 24, 2020
Paris, Ufaransa

TANZANIA YASHIRIKI KWA MARA KWANZA KATIKA MAONESHO YA KIMATAIFA YA BIDHAA ZA KILIMO YA PARIS 2020, UFARANSA

IMG-20200225-WA0006.jpg
Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe. Samwel Shelukindo (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Ujumbe wa Tanzania unaoshiriki


Tanzania inashiriki kwa mara ya kwanza katika Maonesho ya Kimataifa ya Bidhaa za Kilimo ya Paris 2020 yanayofanyika jijini Paris, Ufaransa kuanzia tarehe 22 Februari 2020 hadi tarehe 1 Machi 2020.

Maonesho hayo ambayo yalifunguliwa na Mhe. Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, yanatarajiwa kutembelewa na zaidi ya watu 600,000.

Wakati wa maonesho hayo, Tanzania itapata fursa ya kuonyesha bidhaa zake yakiwemo mazao ya kimkakati. Ujumbe wa Tanzania katika maonyesho hayo unaongozwa na Bw. Victor Rugemalila kutoka TANTRADE.

Ubalozi wa Tanzania ambao unaratibu maonesho hayo kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, unaishukuru Kampuni ya Tanzania Re-assurance (TAN-RE) ya Dar es Salaam, Tanzania, kwa kufadhili kwa kiasi kikubwa ushiriki wa Tanzania katika maonyesho. Aidha, Ubalozi unatambua mchango wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) na Kampuni ya Kahawa ya Inter State.
 
Safi kujitangaza kimataifa kufungua macho ulimwengu wajue huku bongo kuna mambo mazuri sio yule balozi wa kisiasa kutoka chama fulani yeye kutwa ni kutangaza mabaya tu!
 
Au unataka nikuwekee post zako hapa....Ww kama unaipondea hii nchi hama...Nenda S.A huko free Visa maisha mazuri na ushukuru watakachokufanya.


Weka ya huu uzi mbona unanipangia pa kwenda? Wewe vipi?hii nchi sio ya watu fulani ni yetu sote .tusitishane wala kuogopeshana
 
Ww ndo upunguze shobo na ccm yako
Sasa nilivyokwambia unaichukia serikali iliyopo madarakani ulikuwa unakataa nn... Halafu umekariri kila anayesapoti serikali ni ccm... Ngoja tuishie hapa sababu unanipotezea tu muda kigeugeu... Bure kbsa.
 
Back
Top Bottom