Tanzania yashuka viwango vya FIFA

Tanzania yashuka viwango vya FIFA

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598
Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Agosti, 11 limetoa orodha ya timu zinaoongoza kwa ubora duniani na nchi ya Argentina ikiendelea kusalia kileleni ikiwa na alama 1585.

Nafasi ya pili inashikwa na Ubelgiji, nafasi ya tatu Colombia, nafasi ya nne Ujerumani na nafasi ya tano ikishikiliwa na Chile.

Kwa upande wa Tanzania imeshuka kwa nafasi moja kutoka nafasi ya 123 hadi nafasi ya 124 na kwa Afrika Mashariki ikishika nafasi ya 5, nyuma ya Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi.

Aidha viwango hivyo vimeonyesha kuwa kwa Afrika, Algeria inaongoza ikifuatiwa na Ghana, Ivory Coast na Senegal ikishika nafasi ya nne.
 
tukipanda kwa nafasi 24 tutakuwa TOP 100...
 
Na Fikiri kwa mipango na mikakati yenye upembuzi yakinifu waliyonayo viongozi wetu huku wakimtanguliza mungu m'bele tutakuwa namba moja mwakani hatuwezi kuwa mbele ya south sudani tu kwenye ukanda wetu.
 
Tutashindana lakini hatutashinda[emoji23]
 
Waziri nape halafu kule kuna malinzi unapanda VP saaa.
 
Ili tanzania iwini kimichezo ama ifanikishe yatakiwa kujirekebisha mno na iachane na tabia hizi za mauaji ya vikongwe, wezi umekithiri mno,vibaka wametanda kila mahala, ujambazi ndio usiseme...sasa hapo unategemea tanzania italeta matokeo gani mazuri zaidi ya kuporomoka kiuchumi na kimichezo!!! Ni sawa sawa na "kutwanga maji kwenye kinu"


Tanzania tunatakiwa tubadilike.
 
Serikali ndo ilianza kujishusha kufuta michezo mashuleni fifa wanamalizia mshusho
 
Back
Top Bottom