Rashda Zunde
JF-Expert Member
- May 28, 2022
- 204
- 231
Serikali ya Tanzania inakusudia kuongeza kasi na kiwango cha uzalishaji wa mbegu za mafuta ya kula ili kuviwezesha viwanda vya ndani kuzalisha bidhaa hiyo itakayosaidia kuokoa fedha zinazotumika kuagiza mafuta nje ya nchi.
Kutokana na Upungufu wa uzalishaji wa mafuta nchini kwa mujibu wa Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe unatokana na tija ndogo ya uzalishaji ambayo inachangiwa na upatikanaji mdogo wa mbegu bora, mbolea, viuatilifu, matumizi ya mbinu duni za uzalishaji na mabadiliko ya tabianchi.
Mafuta ya kula yanayozalishwa Tanzania yanatoka katika mazao ya alizeti, karanga, pamba, soya, nazi, chikichi na ufuta ambapo, alizeti huchangia asilimia 90 ya uzalishaji wote.
Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/22, Serikali imechukua hatua mbalimbali za kuongeza uzalishaji wa mbegu za mafuta ya kula kwa kusambaza tani 2,000 za mbegu bora za alizeti zenye thamani ya Sh5.8 bilioni kwa utaratibu wa ruzuku kwa wakulima wa mikoa ya Singida, Dodoma, Simiyu na Manyara.
Pia Serikali imeratibu majukwaa 52 ya majidiliano na sekta binafsi kwa mazao asilia ya biashara, nafaka, mikunde, bustani na mbegu za mafuta ya kula kwa ajili ya kutatua changamoto za kikodi na kisera.
Utekelezaji wa mikakati hiyo umeanza kuonyesha matumaini kuelekea katika kupunguza kabisa uagizaji wa mafuta ya kula na kuwawezesha wakulima kuzalisha mbegu za mafuta zitakazokidhi mahitaji yote ya ndani.