Tanzania yatajwa katika suala la Utawala Bora na Usalama

zuujacob

Member
Joined
Dec 10, 2020
Posts
14
Reaction score
10
RIPOTI ya kwanza ya mwaka 2019 ya Mpango wa Afrika wa Kujitathmini Kiutawala bora APRM umebaini Tanzania kufanya vizuri kwenye suala la ulinzi na usalama mambo ambayo yametajwa na ripoti hiyo kuwa yamekuwepo tangu kupata uhuru.

Ripoti hiyo imeipongeza Tanzania katika kusimamia misingi ya haki za binadamu, usalama wa nchi, ukuaji wa uchumi, matumizi ya lugha ya Kiswahili pamoja na kudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa zaidi ya miaka 50 mpaka sasa.

Akizungumza mara baada ya kuwasilisha mada kwenye mkutano wa kitaifa kuhusu ripoti ya Tanzania ya mwaka 2019, Mwenyekiti wa Bodi ya APRM Tawi la Tanzania, Profesa Hasa Mlawa amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizofanya vizuri katika usimamizi wa utawala bora kati ya nchi za Afrika ambazo ni wanachama wa mpango huo
 
Haina shida, kwani waliouawa Tanzania ni ndugu zao?
 
Hiyo taasisi ije ituhoji sisi wananchi wa kawaida kuhusu utawala bora, na sio kusubiri taarifa kwa watawala.
 
Hakuna kipindi nchi imevunja haki za binadamu kama kipindi hiki cha awamu ya tano, sasa hii ripoti ni yakutengeneza. Hawakuona Zanzibar? Lindi( ruangwa)
 
Usalama wa CCM au wananchi wote. Kuna wachekeshaji wengi sana siku hizi mitandaoni
 
Naona wapinzani wametokwa povu.

Wanataka kusikia Tanzania wameidowngrade ndio wako na raha.
 
Timu ufipa wakifika hapa jiandae kuhama nchi😂😂😃.... taarifa hii si njema sana kwa bavicha key board taifa😂😂😂
 
Kumbe huwa hawaangalii parcentage ndogo ya wanaodhurika? mpk nchi iwe kama Afghanistan ndo itaonekana haina haki za binadamu?
Na moto wa nyika huanza na cheche za moto. Report yoyote unayo ihusu Tanzania huhaririwa kabla ya kuandikwa na vyombo vya humu nchini.
 
Tangu lini Umoja wa Afrika -African Union -AU wakalaani matendo maovu ya watawala wa Afrika. APRM wanadai waAfrika wana aina yao maalum ya Demokrasia na Utawala Bora. Kwa maana nyingine APRM na AU-Umoja wa Afrika wanaamini kuwa hata kusipokuwapo uwazi ktk utawala bora ni aina mahsusi ya utawala wa kiAfrika kuficha ukandamizaji, kuumiza, kuchafua chaguzi ili mradi tu kuwepo kitu wanachoita "uzalendo" ambacho kwa macho ya watawala ni kulinda tawala kandamizi kwa gharama yoyote ziendelee kutawala ndiyo usalama wenyewe.

Our Mission​

The mission of the APRM is to promote the African Union’s ideals and shared values of democratic governance and inclusive development by encouraging all Member States of the Union to collaborate and voluntarily participate in the home grown, credible, rigorous, independent and self driven peer review process and the implementation of its recommendations.
Source : About APRM - APRM
 
Wewe ulifanya nini wakati mlipokuwa mnakula keki ya taifa? Maendeleo gani mliyaleta au ndio ulanguzi mliokuwa mnafanya?
 
Watawala mnasingizia ili muweze kuleta Maendeleo kwa nchi , kuwa ni muhimu kwanza kuteka nyara uhuru, haki na maendeleo ya watu.

Mnadai hamtaki "kelele" za vyama vingi kwa kisingizio mtashindwa kuleta Maendeleo hivyo ni muhimu kuua siasa za vyama vingi ili mbaki pekee yenu.

Hamtaki wabunge wa vyama vingine waingie Bungeni kwa kisingizio wa wabunge wa upinzani watachelewesha Maendeleo.

Mnabinya uhuru wa habari kwa kudai hoja mbadala zimejaa 'matusi' haziungi mkono juhudi zimejaa agenda kutetea maruhani mliowapachika jina mabeberu ingawa sote tunajua 'Ruhani' ni kitu cha kufikirika hakipo ktk uhalisia.
 
Watawala mnasingizia ili muweze kuleta Maendeleo kwa nchi , kuwa ni muhimu kwanza kuteka nyara uhuru, haki na maendeleo ya watu.

Mnadai hamtaki "kelele" za vyama vingi kwa kisingizio mtashindwa kuleta Maendeleo hivyo ni muhimu kuua siasa za vyama vingi ili mbaki pekee yenu.

Hamtaki wabunge wa vyama vingine waingie Bungeni kwa kisingizio wa wabunge wa upinzani watachelewesha Maendeleo.

Mnabinya uhuru wa habari kwa kudai hoja mbadala zimejaa matusi.
Wanaochagua ni wananchi, wewe upo upande wa minority. Ile miradi yenu ya ukasuku ya NSSF mlikula bila kunawa mikono. It will never happen again!
 
10 December 2020
Dar es Salaam, Tanzania

Maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu : Kauli-mbiu : Haki Ni Maendeleo

Jaji mstaafu Joseph Warioba mgeni rasmi siku ya haki za binadamu anena kuwa: Afrika kuna maazimio mengi ya kulinda Haki za Binadamu na Demokrasia, lakini wenye mamlaka wamekuwa wagumu, si wasikivu na hawataki kutekeleza maazimio ya haki za binadamu. Tutawasikia viongozi wengi wakitoa hotuba siku ya leo ya maadhimisho Kimataifa Juu ya Haki za Binadamu, tatizo hawasimamii haki hizo toka moyoni mwao.

Nchi za Afrika zimesaini mikataba na maazimio ya mengi ya kikanda, kikontineti (bara la Afrika) na Kimataifa kulinda Uhuru, Haki na Demokrasia lakini hawatekelezi kimatendo hii ndiyo changamoto kwa watawala kutenda walichoahidi ktk mikataba ya kulinda haki za binadamu.

Wakubwa wetu wanatuwakilisha ktk mikutano mingi ya Haki za Binadamu lakini wakirudi ofisini wanakuwa na kigugumizi kutekeleza maazimio.

Vurugu ktk chaguzi Malawi, Mali, Uganda, Zanzibar n.k kutokana na uchaguzi kuvurugwa.

Jaji Joseph Sinde Warioba asema Viongozi wenye mamlaka hulazimisha kuteua viongozi wasiokubalika ktk vitongoji, majimbo ambao hupelekea wananchi kutowatambua na wamewaita "viti maalum". Mawakala wengi wameenguliwa na .......

Source : Mwanachi digital
 
Tujikumbushe 2015 :

Jakaya Kikwete : Umuhimu wa Utawala wa sheria na Haki za Binadamu

Back
Top Bottom