Tanzania yatia aibu huko Olympic

Mkuu ili mwanamichezo wa kada yoyote ashiriki Olympics ni hadi afikie viwango vya kwenda huko...

Riadha, masumbwi na siku za karibuni kuogelea ndio yamekuwa mashindano makuu ambayo Tanzania imekuwa ikitoa wawakilishi...

Kuna mahali nilisoma, Olimpiki ya mwaka huu tutakuwa na wawakilishi wachache sababu hatukuweza kupeleka watu wa masumbwi kwenye qualifications (nadhani Covid ndio kikwazo)...

Hivyo nafasi pekee zilizosalia ni riadha ndio hizo nafasi tatu na kuogelea (kulikuwa na mabwana wadogo wawili sijui kama walifuzu wale)
 
Ahh maamae, huko duniani wanatuona watanzania ni viumbe vya ajabu
 
Watadai hawana hela?! Mpaka tozo za miamala zikubaliwe..
 
Reactions: BAK
Nilikuwa najiuliza watanzania wako wapi kwenye hii olympic kumbe wameenda watatu na hawajulikani walipo. Aibu
Namna ya kuwapata wawakilishi inawezekana ndio tatizo lilipoanzia:
1.Mashindano ya kuwapata wachezaji ,ingehusisha ngazi za wilaya, mikoa hadi Kitaifa.
2.Unaweza kukuta Taarifa ya mashindano ya Olyimpiki haikushirikisha wadau kwa kupanga,kuandaa na kuwaibua washiriki wenye kutimiza vigezo vya ushiriki mashindano husika.
3.Hivi viongozi wa michezo,mmeshindwa hata kuiga kwa jirani(Kenya,Ethiopia na wengine);mfumo wao wa usimamizi na wanafanyaje hadi kuwa na wanamichezo wengi.
4.Waziri wa michezo hapa kuna haja ya kuongeza nguvu ya ufuatiliaji na sera ya michezo kuangaliwa upya.
 
Huyo nu bongo zozo,anaiwakilisha tanzania

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Taifa la watu karibia milioni 60 tumewakilishwa na watu watatu Olympic?!

Nashauri tukapimwe mkojo.
Hv Kuna ulazima gani wakushiriki haya mashindano ikiwa maandalizi ni finyu,si ni Bora kutokushiriki au Kuna ulazima kila nch kushiriki?
 
Hakuna tunachokiweza sisi zaidi yakupiga mdomo nakutishiana kwakutumia mamlaka na vyombo vya dola.Kuanzia raia mmoja mmoja hadi viongozi wakubwa tunachokiweza kwa uhakika ni kuongea ila sio mambo ya kutumia akili au ushindani wowote.Kamwe usitegemee jambo lolote la maana nalakujivunia toka kwa huyu mtu anayetoka kwenye hii ardhi.Na tatizo linaanzia kwa aina ya viongozi tulionao.
 
Nimeumia sana kwa tukio hilo mkuu The Genius ,lakini nimeumia sana zaidi kwa hayo maandishi yako mkuu.
Umeandika ukweli mtupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…