Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
Tanzania yatoa tahadhari dhidi ya ugonjwa wa ebola
Wizara ya Afya nchini Tanzania imewashauri wananchi wake kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa ebola siku moja baada ya nchi jirani ya Uganda kuthibitisha mlipuko mpya wa virusi vya ugonjwa huo.
Naibu Waziri wa afya Dk Godwin Mollel imewaelekeza Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri nchini kuimarisha utoaji wa elimu, ufuatiliaji wa ugonjwa, uchunguzi wa kitaalam na kuhakikisha upatikanaji wa vifaa tiba na kinga muhimu katika maeneo yao.
"Vilevile, nimewaelekeza kuimarisha uchunguzi wa wageni wanaoingia nchini kupitia mipaka yetu ikiwemo matumizi ya vipima joto" ilisema taarifa hiyo.
Hata hivyo amewataka wananchi kuchukua tahadhari ikiwa ni pamoja na kunawa mikono kwa maji safi na sabuni, kuepuka kugusa mwili au majimaji ya mwili wa mhisiwa au mgonjwa wa Ebola na kuepuka safari zisizo za lazima kutembelea maeneo yaliyoathirika na ugonjwa huo September 20.
Uganda ilithibitisha mlipuko wa virusi vya Ebola baada ya mwanaume mwenye umri wa miaka 24 aliyeambukizwa Ebola kufariki dunia katika mlipuko mpya uliothibitishwa na maafisa wa afya. https://www.bbc.com