Tanzania yavunja rekodi kuwa nchi ya kwanza kusimika Intaneti katika kilele kirefu zaidi cha mlima

Tanzania yavunja rekodi kuwa nchi ya kwanza kusimika Intaneti katika kilele kirefu zaidi cha mlima

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Siku ya jana katika maazimisho ya siku ya uhuru waziri wa habari na mawasiliano alifanikiwa kuzindua internet yenye kasi zaidi katika kilele cha Mlima kilimanjaro chenye urefu wa mita 5,895kutoka usawa wa bahari.

Huduma hii ya internet ni sehemu ya kuifungua zaidi Tanzania katika Nyanja za utalii ambapo watalii kutoka katika mataifa mbalimbali sasa wanaweza kupata huduma ya internet yenye kasi zaidi.

Kutokana na kufanikiwa kuwepo kw ainterneti katika mlima kilimanjaro Tanzania itakuwa nchi ya kwanza kusimika huduma ya internet katika kilele kirefu zaidi barani afrika.

Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu inaendelea kuimarisha na kuboresha utalii Tanzania maana utalii ni moja kati ya sekta inayochangia kwa kiasi kikubwa pato la Taifa.
 
Huko Chama Cha Mambuzi kuna vijana wa ovyo sana

Vijana wasiojua ili kushindanisha lazima wanaoshindanishwa wawe na vigezo linganifu! Ndio hawa hulinganisha nanasi na chungwa kwa kitamu!! Hawajui nanasi zitalinganishwa peke yake na machungwa peke yake labda kwa maeneo bidhaa hizo zinakotoka. Si sahihi kusema “nanasi tangu kuliko chungwa”. Ni sahihi kusema “nanasi ya tanga tamu kuliko ya geita”!!

Nchi imejaa vijana wa hovyo, siku wakipungua itasonga mbele!!
 
Siku ya jana katika maazimisho ya siku ya uhuru waziri wa habari na mawasiliano alifanikiwa kuzindua internet yenye kasi zaidi katika kilele cha Mlima kilimanjaro chenye urefu wa mita 5,895kutoka usawa wa bahari.

Huduma hii ya internet ni sehemu ya kuifungua zaidi Tanzania katika Nyanja za utalii ambapo watalii kutoka katika mataifa mbalimbali sasa wanaweza kupata huduma ya internet yenye kasi zaidi.

kutokana na kufanikiwa kuwepo kw ainterneti katika mlima kilimanjaro Tanzania itakuwa nchi ya kwanza kusimika huduma ya internet katika kilele kirefu zaidi barani afrika.

Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu inaendelea kuimarisha na kuboresha utalii Tanzania maana utalii ni moja kati ya sekta inayochangia kwa kiasi kikubwa pato la Taifa.
Mburumundu...
 
Mama kanyaga twende tumecheleweshwa mnooo kama taifa zaidi ya miaka 6
 
Anatuona wote ngumbaru
Duh mawazo mengine, kabla ya kuandika thread hii umejiuliza ni nchi ngapi zina milima mrefu kama Kilimanjaro ulitaka Burundi iwe ya kwanza kusimika je ina mlima mrefu?
 
Sasa imekuwa nchi ya kwanza kusimika Intanet katika mlima kilimanjaro kwani Kuna kilimanjaro ngapi duniani?Ama mlima kilimanjaro unamilikiwa na nani?.Kwa hiyo Tanzania imetimiza wajibu wake Kwa sababu hamna kilimanjaro nyingine inayoshindana nayo.
 
Duh mawazo mengine, kabla ya kuandika thread hii umejiuliza ni nchi ngapi zina milima mrefu kama Kilimanjaro ulitaka Burundi iwe ya kwanza kusimika je ina mlima mrefu?
Toka lini chawa akawa na akili?...hawa ndio vijana waliopo sasa.
Hili ni jambo zuri ila kwa sababu ni chawa kaona alilete hivi....
 
Mount Everest walisimika tena sio moja zipo zaidi ya 30 4g
Tangu simu zimeanza Duniani
leo ndio mmeshtuka na kusifu

Tunajua upigaji, ungeweka na gharama
Au mnasubiri moto mseme mnara uligharimu mabilioni
 
Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu inaendelea kuimarisha na kuboresha utalii Tanzania
Hapo tu ndo tatizo lilipo anzia thread nzuri ila mwishoni imekaa kichawachawa tu
 
Duh mawazo mengine, kabla ya kuandika thread hii umejiuliza ni nchi ngapi zina milima mrefu kama Kilimanjaro ulitaka Burundi iwe ya kwanza kusimika je ina mlima mrefu?

Upo sahihi,sa hivi tumekua na kizazi cha ovyo sana,na uwezo wa kufikiri umepungua.kizazi cha kusifia upumbavu
 
Back
Top Bottom