Tanzania yazidi kuporomoka viwango vya soka FIFA

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
Tanzania imeporomoka kwa nafasi tano kwenye viwango vya shirikisho la soka duniani, FIFA kwa mwezi Novemba.

Taarifa iliyotolewa na FIFA inaonyesha Tanzania inashika nafasi ya 147 kutoka ya 142 mwezi Oktoba, wakati Uganda imeendelea kuongoza katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, ikiwa inashika nafasi ya 75 duniani – na Senegal inaendelea kuongoza kwa Afrika nzima ikiwa inashika nafasi ya 23 FIFA.

Katika 10 Bora mwezi huu Ujerumani bado inaongoza ikifuatiwa na Brazil, Ureno, Argentina, Ubelgiji, Hispania, Poland, Uswisi, Ufaransa na Chile.
 
Umewahi sana kuleta taarifa mi nasubiri siku itakayokuwa ya mwisho kabisa maana kinachoendelea kwa sasa kwenye soka la bongo ni upuuzi haiwezekani mtu avunje kanuni harafu wasimamia kanuni wanasema busara itumike
 
Hizi takwimu zingekuwa zinatolewa na magu or NBS ungesikia wanasema tanzania imepanda na wanaodai imeshuka ni wenye vyeti feki na wapiga dili wakamatwe na wafungwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…