Tanzania yazindua Tanzania Power Interconnector Project kwa ajili ya kuuza umeme kwenye nchi za EAC na SADC

Tanzania yazindua Tanzania Power Interconnector Project kwa ajili ya kuuza umeme kwenye nchi za EAC na SADC

diana chumbikino

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
428
Reaction score
368
8676a72cf3d3375b24fc65e3b5a5bc8d.jpg

Tanzania imeanza utekelezaji wa mradi mkubwa wa mabilioni ya Shilingi wa kuunganisha umeme kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na zile za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambao ukikamilika, nchi itauza umeme mwingi nje.

Mradi huo pia utakuwa na faida nyingi zikiwamo kuongeza usambazaji kwa mikoa ya kusini mwa Tanzania na kuimarisha uwezo wa taasisi nchini katika biashara ya umeme.

Pia utazisaidia nchi za Kenya na Tanzania kuondokana na umeme wa gharama kubwa unaofuliwa kwa gesi na kutumia wa gharama nafuu wa maji, hivyo kupunguza uchafuzi wa kemikali zinazotokana na gesi.

Mradi huo unafahamika kwa jina la Kenya – Tanzania Power Interconnector Project (KTPIP)/ZTK au Mradi wa Laini ya Msongo wa Kilovolti 400 wa Isinya – Namanga – Singida, utakaokamilika mwakani.

Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari katika mojawapo ya eneo la mradi, Kijiji cha Nanya Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, mratibu wa mradi huo, Peter Kidagye alisema gharama za mradi ni Dola za Marekani milioni 258.82 (takribani Sh bilioni 600).

Kidagye anayefanya kazi Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) alisema mradi unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Japan (JICA), Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) na Serikali ya Tanzania.

Alisema mradi huo ni sehemu ya mpango wa maendeleo ya sekta ya nishati ambao Serikali ya Tanzania inakusudia kuunganisha Gridi ya Taifa na nchi za Kenya na Zambia.

Katika mpango huo, alisema utaiwezesha Tanzania kuingiza umeme wa bei rahisi kutoka Ethiopia kupitia Kenya hadi Zambia kwa mpango unaojulikana kama Southern African Power Pool (SAPP).

Alieleza kuwa mradi huo wa KTPIP utakuwa na urefu wa kilometa 510.7, na kati ya hizo, Tanzania itakuwa na kilometa 414.7 na Kenya kilometa 96. Alisema utaanzia mkoani Singida kutoka katika mradi mwingine mkubwa nchini maarufu kama Backbone, ambao utaunganishwa kupitia Babati – Arusha – Namanga hadi Isinya, Kenya.

Alisema tayari kipande cha Singida hadi Babati (kilometa 150), mkandarasi ni Kampuni ya Kalpataru Power Transmission ya India kwa gharama ya dola za Marekani milioni 34.84 na Sh bilioni 17.982.

Kwa kipande cha Babati hadi Arusha cha kilometa 150, mkandarasi ni Bouygues Energies & Services (BYES) ya Ufaransa kwa gharama ya dola milioni 36.89 na Sh bilioni 22.354. Kipande cha tatu kuwa ni Arusha hadi Namanga mpakani na Kenya chenye urefu wa kilometa 114.7, kinachojengwa na kampuni za Energoinvest & EMC (CEE) kutoka Bosnia- Herzegovina na India, kwa gharama ya dola milioni 30.65 na Sh bilioni 18.97.


Mratibu wa mradi kutoka Tanesco alieleza kuwa pia kutakuwa na ujenzi wa kituo cha kupooza umeme cha kilovolti 400 Lemugur jijini Arusha na ukarabati wa kingine cha Singida cha kilovolti 220/33.

Alifafanua kuwa Serikali ya Tanzania imelipa dia ya dola za Marekani milioni 40 (zaidi ya Sh milioni 80) kwa wananchi walioathiriwa na mradi huo. Kwa upande wake, Meneja Mwandamizi wa Miradi wa Tanesco, Emmanuel Manirabona alieleza kuwa vifaa kwa ajili ya mradi huo vimeshawasili na makandarasi wanaendelea na kazi yao vizuri.

Wahariri wameshuhudia mkandarasi Kampuni ya Bouygues Energies & Services pamoja na wafanyakazi wake wakiendelea na kazi ya kumwaga zege kwa ajili ya kusimika minara ya umeme ambao kwa kipande cha Babati – Arusha itakuwa 383.

Meneja Mkazi wa mradi wa kampuni hiyo ya Kifaransa, Christopher Bartholome alisema wanatarajia kukamilisha kazi hiyo kwa wakati kwani wamekamilisha vifaa vyote, na pia wasingependa kutozwa faini kwa kuchelewesha kazi.
 
Fakeni!!25% ya wananchi ndio wana umeme. Halafu unapiga promo kuuza nje.
 
Lile bomba la mafuta kutoka nchi jirani ujenzi umeshaanza...? Uzinduzi ulikuwa na mbwembwe sana, hii ni dona kantrii.... Usiku Utapokwisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom