Tanzania yazindua Ubalozi na uwakilishi wa kudumu nchini Austria

Tanzania yazindua Ubalozi na uwakilishi wa kudumu nchini Austria

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imezindua rasmi Ubalozi na Uwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa jijini

Vienna nchini Austria.

Akizungumza katika uzinduzi huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) amesema kufunguliwa kwa Ubalozi huo ni mafanikio yanayoimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya

Tanzania na Austria na Taasisi za Umoja wa Mataifa zilizopo jijini Vienna na kinaonesha jinsi Tanzania inavyoipa kipaumbele Austria.

"Kufunguliwa kwa Ubalozi huu ni mafanikio makubwa ambayo yanaimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya

Tanzania na Austria na Taasisi za Umoja wa Mataifa zilizopo hapa jijini Vienna na kinaonesha kwa vitendo kuwa

Tanzania inaipa kipaumbele Uhusiano wake na Austria, alisema Dkt. Tax.

Ameishukuru Serikali ya Austria na Wizara inayoshughulikia masuala ya Ulaya na uhusiano wa Kimataifa kwa ushirikiano mkubwa ambao imekua ikiupatia Ubalozi wa Tanzania

Vienna tangu ulipoanzishwa hadi kufikia siku ya uzinduzi.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Ubalozi huo jijini

Vienna Naibu Waziri anayeshughulikia Masuala ya Ulaya na

Uhusiano wa Kimataifa Mhe. Peter Launsky-Tieffenthal amesema Austria inapongeza uamuzi wa Serikali ya Tanzania wa kufungua Ubalozi wake Austria na kuungana na nchi nyingine 16 za Afrika zenye Ubalozi nchini humo na kuahidi kuusaidia Ubalozi huo kwa kila hali ili kufikia malengo ya kuanzishwa kwake.

"Austria inapongeza uamuzi wa Serikali ya Tanzania wa kufungua Ubalozi wake Austria na hivyo kuungana na nchi nyingine 16 za Afrika ambazo zina Balozi zao hapa nchini, niwa ahidi na kuwahakikishia kuwa Serikali ya Austria iko tayari kuusaidia Ubalozi huo kwa kila hali ili ufikie malengo ya kuanzishwa kwake", alisisitiza Waziri huyo.

DC2417A4-AA9A-4A3B-B8A4-5E343E4F7529.jpeg
 
Back
Top Bottom