SoC04 Tanzania yenye mandhari nzuri, muonekano safi na utunzaji wa mazingira

SoC04 Tanzania yenye mandhari nzuri, muonekano safi na utunzaji wa mazingira

Tanzania Tuitakayo competition threads

NYANOHA

Member
Joined
Sep 2, 2022
Posts
5
Reaction score
4
Tumekua tukitamani na sisi nchi yetu iwe kama nchi za ulaya kimuonekano, kwani zina nuonekano mvuri, mandhari nzuri na mazingira safi, hata sisi tunaweza kuifanya Tanzania yetu ionekane kama nchi hizo.

Kwa ushirikiano wa serikali, wawekezaji na jamii nzima kupitia sera zenye maono na utekelezaji thabiti, tunaweza kufanikisha mkakati huu wa kuipata Tanzania yenye mandhari nzuri, mazingira safi na maisha bora kwa wote kwa kufanya yafuatayo.
  • Sera za ujenzi wa nyumba za kisasa nchi nzima. Ili kufanikisha dhamira yetu ya kuijenga Tanzania yenye mandhari nzuri basi tunatakiwa tujenge nyumba za kisasa “flat roof” na sio nyumba tulizozizoea au kurithi kwa waezee wetu za mapaa ya bati, makuti au vigae, nyumba za aina hii hazihitajiki tena, hivo basi tuweke sera ambayo itakua ndio muongozo kwa yoyote anaetaka kujenga basi sharti afate muongozo huo iwe serikali, muwekezaji au raia kwa kile anachataka kukijenga, iwe offisi, duka, nyumba, hoteli, skuli, hospital, kanisa, msikiti, madrasa nk.​
Tuangalie picha zifuatazo zikiwa na pendekezo la ujenzi husika.

Mjini tujenge nyumba kama hizi kwenye picha,

ghor.jpg


mjin.jpg
Chanzao cha hizo ni shurtterstock.com

Hotel zujengwe kama hizi.
hotl.jpg

hotel.jpg
Chanzo cha picha ni ebhosworkd na arcmaxarchitect.

Nyumba za raia na offisi ndogondogo zijengwe kama hizi.
raia.jpg

ria.jpg
Chanzo cha picha ni muthurwa.com

Skuli zijengwe kama hizi.
photo_2024-05-05_15-00-35.jpg

photo_2024-05-05_15-00-48.jpg

Chanzo cha picha ni hctraft na depositphotos.

Hospital zijengwe kama hizi.
photo_2024-05-05_15-00-18.jpg

Chanzo cha picha ni design square.

Misikiti ijengwe kama hii.
photo_2024-05-05_14-59-51.jpg

photo_2024-05-05_15-00-55.jpg

Chanzo cha picha ni idei.club na behance.

Makanisa yajengwe kama haya.
photo_2024-05-05_15-00-04.jpg
photo_2024-05-05_14-59-57.jpg

Chanzo cha picha ni pinterest na systegra broup.


  • Tujenge barabara za kisasa “8 lane highway” nchi nzima. Kujenga barabara za 8 lane highway nchi nzma, ambazo zina upana mkubwa wa barabara, zina umuhimu mkubwa katika kuboresha mandhari ya nchi ya kuvutia na muonekano bora. Barabara hizi zinakua zimejengwa kisasa na kuzingatia vipaumbele vya usalama kama vile njia maalum kwa wapanda baiskeli, njia za watembea kwa miguu, na njia za magari ya dharura. Hii inapunguza ajali za barabarani na msongamano wa magari na kuongeza usalama wa watumiaji wa barabara​
.​
Picha zifuatazo zinatonyesha barabra hizo zinaonekanaje.​

lane.jpg
lane.jpg
chanzo cha picha hizi ni shutterstock.com​

Pia barabara hizi zinatakiwa ziambatane na vitu vifuatavyo ili kuongeza mvuto zaid na mandhari nzuri.​
  1. Vituo vya kupakia na kushusha abiria. Ili kuziongezea barabara hizi muonekano mzuri basi ni lazima kujengwe vituo vya kupakia na kushusha abiria vya kisasa, katika kuongeza jambo la ziada basi nashauri vijengwe na vyoo katika kila kituo.
Tuone kupitia picha mfano wa vtuo hivyo.​
bs e.jpg
Chanzo cha picha ni yahoo news Singapore.​
2. Sheli. Pia tunalazimka kujenga sheli za kisasa za kuvutia kila baada ya kilomita moja na ziwe na huduma ya ATM.

shel.jpg
sheli.jpg
Chanzo cha piacha ni pinterest.com​
  • Kujenga miji midogo midogo ya kisasa miwili kwa wilaya. Pia baada ya kujenga mijengo ya kisasa tunatakiwa kujenga miji midogomidogo ya kisasa nje ya miji ili kuipa haiba nchi na kuongeza nguvu katika kuijenga Tanzania yenye kupendeza na kuvutia, mfano wa miji kama hii ni fumba town unaopatikana zanzibar. Kama unavoenekna katika picha ziilizopo chini.
    fumb.jpg
    fmb.jpg
  • Chanzo cha picha ni issuu na indian memon​

    • Kujenga garden parks angalau 3 kila wilaya. Hizi ni sehem ambazo kunakua na sehem za kukaa zikiwa zimezunguukwa na bustani iliyo pandwa na kubuniwa kwa ustadi wa hali ya juu kabisa ili kulipendezesha eneo hilo na kuwavutia watu kwenda kupumzika au hata kuliona tu kutokana na mvuto wake. Mfano wa gardens hizo ni kama forodhani, jamhuri na botanic garden zote zikiwa zinapatikana zanzibar. Tuangalie picha zifuatazo kuona jiinsi gan zinavokua.
      gard.jpg
      garden.jpg
      jmr.jpg
      Chanzo cha picha ni alamy, flickr na mtaa kwa mtaa blog.
  • Kujenga miundombinu ya umeme ya kileo. Nchi yetu bado inatumia miundombinu za kizamani ya umeme ambayo imekua ikichafua mandhari na muonekanao wa nchi hivo basi kwa kua tunahitaji kujenga Tanzania ya kisasa yenye mandhari nzuri na muonekano bomba basi hatuna budi kuhama kutoka miundombinu ya zamani na kuja katika miundombinu ya kisasa ambayo nayo itachangia kwa kiasi Fulani katika kuijenga Tanzania ya kuvutia kimuonekano. Hem tuangalie kupitia kwenye picha zifuatazo miundimbinu hiyo inayo hitajika.​
  • umem.jpg
  • Chanzo cha picha ni Carolina country.​
  • Kujenga sehem za kufurahishia watoto. Vituo vya kufurahishia watoto vinaenda kuongeza nguvu kwenye sera ya nchi ya kuijenga tazania yenye mvuto na muonekano mvuri wa kuvutia kwani vituo hivi vinakua na aina nyingi za michezo ambayo mtu akiiona tu lazima moyo wake ushangae na kujisemea kimoyomoyo “hivi hii ni Tanzania kweli”. Mfanowa vituo kama hivi vinapatikana kariakoo zanzibar na verde hotel zanzibar.​
  • Utunzaji wa mazingira. Baaada ya kufanikisha kujenga mambo yote katika kiundombinu ya kisasa kinachofuata ni kuwa na kampeni ya kutunza mazingira kuanzia serikalini, wawekezaji na raia kwa ujumla, lazima kuwepo na ushirikiano wa kweli baina ya pande hizi tatu ili kufanikisha suala hili la kutunza mazingira. Sera ya kutunza mazingira nchi nzima inatikiwa iwe kama ifuatavyo.​
    1. Kuwekwe madebe ya takataka pembezoni mwa barabara zote nchi nzima ili watumiaji wa barabara wawe wanatia takataka humo.
      dust.jpg
      dustphoto_2024-05-05_14-14-09.jpg
    2. Chanzo cha picha ni dreamstime.com na 123rf.​
    3. Kila nyumba lazima iwe na madebe ya takataka mawili kwa lengo la kuziweka takaka zote humo na baaadae kuzipeleka katika sehem zilizotengwa katika maenoe hayo.​
    4. Kutenga sehemu maalumu kwa ajili ya takataka zinazopatikana majumbani ili wananchi baada ya madebe yao kujaa basi wazipeleke katika sehem hizo ambazo manispaa au kampuni za kuhifadhi watapita kila baada yamda kuzichukua na kuzipeleka zinakotakiwa.​
    5. Kutungwa kwa sharia ndogondogo za kutunza mazingira ili mtu yoyote atakaevunja sheria kwa kutupa takataka nje ya madebe basi aadhibiwe.​
    6. kuanzisha mipango ya kidhibiti uchafuzi wa hewa, maji na ardhi kwa kuhimiza matumizi ya magari yanayotumia nishati endelevu na kuhamasisha mbinu za kisasa za usimamizi wa taka ni muhimu katika kudumisha mazingira mazuri nchi.​
    7. Kuwekwe utaratibu wa kuwapa zawadi watu wanaongoza kwa kutunza mazingira, watumishi watakao wajibika ipasavyo katika majukumu yao, mitaaa, wilaya au mikoa,itakayoongoza kwa utunzaji wa mazingira, hii itashajihisha watu katika suala zima la kupenda kutunza mazingira na baadae kuona ni jambo la kawaida katika maisha ya kila siku bila y ahata kushrutishwa na utawala.​
Mpaka hapo tutakua tayari tumeshaipata na kuijenga ile Tanzania ya ndoto zetu yenye mandhari nzuri ya kuvutia na utunzaji wa mazingira.
 

Attachments

  • photo_2024-05-05_14-59-57.jpg
    photo_2024-05-05_14-59-57.jpg
    100.5 KB · Views: 5
  • 8 lane.jpg
    8 lane.jpg
    27 KB · Views: 7
Upvote 2
Sera za ujenzi wa nyumba za kisasa nchi nzima. Ili kufanikisha dhamira yetu ya kuijenga Tanzania yenye mandhari nzuri basi tunatakiwa tujenge nyumba za kisasa “flat roof” na sio nyumba tulizozizoea au kurithi kwa waezee wetu za mapaa ya bati, makuti au vigae, nyumba za aina hii hazihitajiki tena, hivo basi tuweke sera ambayo itakua ndio muongozo kwa yoyote anaetaka kujenga basi sharti afate muongozo huo iwe serikali, muwekezaji au raia kwa kile anachataka kukijenga, iwe offisi, duka, nyumba, hoteli, skuli, hospita
Mi kwenye muonekano sina ubaya nazo wala. Wajenge wanavyojua, waweke paa zitakazowavutia ila tu ziwe standard. Nyumba tunamokuzia watoto lazima ziwe na ubora kwa afya zao na akili njema.

Lakini tu kwenye ubora. Tuwe na kitu kama TBS kinachodhibiti ubora wa nyumba. Mfano mtu akisema hii ni nyumba ya kuishi ya kupangisha, basi iwe na sifa hizo na kufaa.

Iwe tu kama ilivyo kwenye fremu za maduka ya dawa, kuna sheria inayozitaka ziwe namna fulani na sifa fulani. Basi hilo lisambae hadi kwenye Day care, Fremu, nyumba za kupanga na kadhalika. Mtindo wa kushonanisha fremu tu na hatujui watu watajisaidia wapi mfano, ukomeshwe.

Skuli zijengwe kama hizi.
Mashuke na taasisi ni sawa kabisa kuwa za ghorofa kama mdau mmoja alivyosisitiza
Kujenga garden parks angalau 3 kila wilaya. Hizi ni sehem ambazo kunakua na sehem za kukaa zikiwa zimezunguukwa na bustani iliyo pandwa na kubuniwa kwa ustadi wa hali ya juu kabisa ili kulipendezesha eneo hilo na kuwavutia watu kwenda kupumzika au hata kuliona tu kutokana na mvuto wake
Hii nzuri hata kwa kuzituliza afya za akili za watu. Maua.

Ahsante
Kuwekwe madebe ya takataka pembezoni mwa barabara zote nchi nzima ili watumiaji wa barabara wawe wanatia takataka humo.
dust.jpg
Hakika tunahitaji kuanza kujenga utamaduni wa kuchakata tena na 'upcycling' pia. Insha ni njema✔ na tena hata kabla hatujaiwazia nchi kujenga yote hayo.

Kila mmoja aanze na kwake, nyumbani kwako panakuwa standard kadri inavyowezekana. Mfano umekosa jiko la kisasa, kweli hata kupanda maua ushindwe?
 
Mi kwenye muonekano sina ubaya nazo wala. Wajenge wanavyojua, waweke paa zitakazowavutia ila tu ziwe standard. Nyumba tunamokuzia watoto lazima ziwe na ubora kwa afya zao na akili njema.

Lakini tu kwenye ubora. Tuwe na kitu kama TBS kinachodhibiti ubora wa nyumba. Mfano mtu akisema hii ni nyumba ya kuishi ya kupangisha, basi iwe na sifa hizo na kufaa.

Iwe tu kama ilivyo kwenye fremu za maduka ya dawa, kuna sheria inayozitaka ziwe namna fulani na sifa fulani. Basi hilo lisambae hadi kwenye Day care, Fremu, nyumba za kupanga na kadhalika. Mtindo wa kushonanisha fremu tu na hatujui watu watajisaidia wapi mfano, ukomeshwe.


Mashuke na taasisi ni sawa kabisa kuwa za ghorofa kama mdau mmoja alivyosisitiza

Hii nzuri hata kwa kuzituliza afya za akili za watu. Maua.

Ahsante

Hakika tunahitaji kuanza kujenga utamaduni wa kuchakata tena na 'upcycling' pia. Insha ni njema✔ na tena hata kabla hatujaiwazia nchi kujenga yote hayo.

Kila mmoja aanze na kwake, nyumbani kwako panakuwa standard kadri inavyowezekana. Mfano umekosa jiko la kisasa, kweli hata kupanda maua ushindwe?
Thanks
 
Back
Top Bottom