SoC04 Tanzania yenye Miji safi, barabara salama na kiwango cha chini cha uhalifu kwa msaada wa teknolojia ya kamera za uchunguzi (Surveillance Cameras)

SoC04 Tanzania yenye Miji safi, barabara salama na kiwango cha chini cha uhalifu kwa msaada wa teknolojia ya kamera za uchunguzi (Surveillance Cameras)

Tanzania Tuitakayo competition threads

Goldenmind

Member
Joined
May 22, 2024
Posts
10
Reaction score
9
images (69) (1).jpeg

Chanzo: Latest news and case studies

Utangulizi

Tanzania ni nchi iliyojengwa kwa taswira ya amani na usalama kwa raia. Hii imepelekea nchi yetu kutambulika kama kisiwa cha amani. Licha ya sifa hizi nzuri, tafiti za hivi karibuni zinaonyesha kwamba ukuaji wa kasi wa miji na majiji yetu umechangia kuongezeka kwa matatizo kama uhalifu, ajali za barabarani na uchafuzi wa mazingira.

Mchekeshaji maarufu nchini Marekani Dave Chappelle, aliwahi kusema "Matatizo ya kisasa yanahitaji ufumbuzi wa kisasa." Wakati umefika sasa kutatua matatizo yanayoikabili nchi yetu kwa kutumia teknolojia za kisasa. Matatizo kama uhalifu, ajali za barabarani na uchafuzi wa mazingira yanaweza kutatuliwa kwa msaada wa kamera za uchunguzi.

Kamera za uchunguzi ni nini?
Kamera za uchunguzi ni kamera za video zinazotumiwa kwa madhumuni ya kutazama eneo. Kamera hizi mara nyingi huunganishwa kwenye kifaa cha kurekodi au mtandao wa IP na zinaweza kutazamwa na mwendeshaji au afisa wa kutekeleza sheria.

Aina za camera
Zipo aina mbalimbali za kamera za uchunguzi kama ifuatavyo:

  • Kamera za utambuzi wa nambari za sahani za Leseni (License Plate Recognition)
  • Kamera za pan-tilt-zoom
  • Smati kamera zitumikazo kutambua sura na kufatilia mienendo ya watu au vitu
  • Kamera za infrared zenye uwezo wa kunasa matukio katika mwanga hafifu, usiku au hali mbaya ya hewa

Hanwha_Wisenet (1).jpg

Chanzo: Video Surveillance Archives

Ufungwaji

Kamera za uchunguzi hufungwa nje ya majengo au kwenye nguzo za taa za barabarani urefu wa mita tatu mpaka tano. Manispaa, miji na majiji mengi ya Tanzania yamefanikiwa kufunga taa za barabarani zinazotumia nishati ya jua na hivyo kurahisisha uwekaji wa kamera zitazotumia nishati ya jua pia.

surveillance-cctv-cameras-mounted-post-samara-russia-may-against-blue-sky-147970362.jpg

Chanzo: Dreamstime.com


Jinsi mfumo unavyofanya kazi
Kamera za uchunguzi hurekodi na kutuma video kwenda chumba cha kudhibiti kwa kutumia miunganisho ya waya (kebo za Ethaneti), miunganisho isiyo na waya (Wi-Fi), au mifumo maalumu ya CCTV. Waendeshaji katika chumba cha kudhibiti hufuatilia mipasho hii kwa madhumuni ya usalama na ufuatiliaji.

Uendeshaji wa mfumo
Vijana wa kitanzania wenye taaluma ya kompyuta, habari na teknolojia (Computer & IT) watapata fursa za ajira kuendesha mifumo hii. Ajira hizi zitasaidia kupunguza wimbi la vijana wenye taaluma wasio na ajira au waliojiajiri kwenye sehemu zisizo rasmi kama mabanda ya kuchoma CD au kuweka nyimbo.

images (68) (1).jpeg
Chanzo: nbcnews.com/ Control Room


FAIDA ZA KAMERA ZA UCHUNGUZI


A. Kudhibiti uvunjifu wa sheria za usalama barabarani
Ajali zimesababisha vifo na kuzima ndoto za watu wengi huku zikiwaacha wengi zaidi wakiwa walemavu, tegemezi na ombaomba. Kamera za uchunguzi zitasaidia kuboresha usalama barabarani kama ifuatavyo:
  • Kunasa ushahidi utaotumika kuwawajibisha madereva wazembe waendeshao mwendo mkali, wasababishao ajali na kukimbia eneo la tukio (hit and run), wavunjao sheria makusudi kama kupita njia za mwendo kasi, kutosimama inapoonyeshwa taa nyekundu au kwenye alama za vivuko.​
  • Kuwatia hofu madereva kutovunja sheria za usalama barabarani kwa kuamini wanaonwa na kamera.​
  • Kuwapunguzia afisa usalama barabarani ugumu wa kazi na kupunguza mianya ya rushwa.​
  • Kuwapatia polisi taarifa sahihi za vyanzo vya ajali ili kulinda madereva wasio na hatia na kuwezesha maboresho ya mikakati ya kudhibiti ajali.​
  • Kuwawezesha polisi kudhibiti suala zima la foleni barabarani na kufatilia maeneo hatarishi kama madaraja yaliyofurika ili kuyafunga na kuzuia maafa.​

B. Kudhibiti uchafuzi wa mazingira
Licha ya mamlaka kupambana kuhakikisha majiji na miji yetu inakua safi bado kumekuwa na changamoto kubwa ya usafi. Majiji kama Dar es Salaam yamegubikwa na harufu mbaya inayotokana na taka zilizorundikwa kwenye hifadhi za barabara.

Teknolojia ya kamera za uchunguzi ina ufanisi mkubwa kudhibiti uchafuzi wa mazingira kuliko mabango kwani huweza:
  • Kuwatia hofu wenye nia ya kuchafua mazingira kwa kuwafanya wahisi wanaonwa na kamera.​
  • Kutambua watupaji taka ovyo: kamera za uchunguzi zikiunganishwa na mifumo ya utambuzi kama NIDA, zinao uwezo wa kutambua sura na taarifa za wachafuzi mazingira. Taarifa hizi zitatumika kama ushahidi inapobidi kuwawajibisha wachafuzi mazingira.
    Angalizo:
    Hatua hii itahusu wale wanaotupa taka maeneo yasiyo rasmi. Hii ni baada ya mamlaka kutenga maeneo maalum kwa ajili ya ukusanyaji taka na utaratibu mzuri wa kuziondoa.​

30072009334.jpg blog (2).jpg

Chanzo: Magangam.blogspot.com

100_2339.JPG

Chanzo: hatimes.blogspot.com/ Mwenge mataa


  • Kamera za uchunguzi zikiunganishwa na mifumo ya halmashauri za majiji zitawezesha halmashauri hizi kupata taarifa za maeneo yenye taka zinazohitaji kuondolewa kwa haraka. Hii itawezesha taka kuondolewa haraka tofauti na mifumo ya awali ya kupitisha magari ya kuzoa taka kwa ratiba.​

WY130024 (1).JPG

Chanzo: hatimes.blogspot.com/ moshi

C. Kudhibiti uhalifu
Katika majiji yetu kumekuwa na kukithiri kwa matukio ya kihalifu kama:

  • Wizi wa vyombo vya moto (magari au pikipiki)
  • Wizi wa kutumia pikipiki kukwapua simu, mikoba na vitu vya thamani vya watembea kwa miguu au kuvamia maeneo ya biashara kupora na kukimbia
  • Watu kutekwa, kuporwa na kupotezwa na vikundi vya wahalifu kama “watu wasiojulikana” au “panya rodi”

Kamera za barabarani zitasaidi kupunguza kiwango cha uhalifu katika maeneo mbalimbali kama ifuatavyo:
  • Kamera za uchunguzi zitawarahisishia polisi uchunguzi wa uhalifu na kuwapatia taarifa za kijasusi kuhusu upangaji na utekelezaji matukio wa vikundi vya wahalifu, kuwatambua wahalifu na kuwawezesha kuwasili kwa wakati maeneo ya matukio ili kuzuia uhalifu kabla haujafanyika.​
images (67) (2) (2).jpeg

Chanzo: facebook.com/susatule/panyarodi


  • Pia kamera za uchunguzi zitatumika katika ushahidi mahakamani ili kuharakisha uchunguzi na kuwalinda wasio na hatia. Endapo unashutumiwa kimakosa, kamera za uchunguzi zinaweza kutoa ushahidi wa video kuwa hukuwepo eneo la tukio au hukufanya uhalifu.​

Changamoto
1. Udukuzi wa mifumo

Mifumo ya kamera za ufuatiliaji huweza kudukuliwa na kupelekea kuhatarisha uadilifu na usiri wa video zilizonaswa.
2. Faragha
Matumizi ya kamera za uchunguzi huibua wasiwasi kuhusu ukiukaji wa faragha, kwani watu binafsi wanaweza kuhisi wasiwasi kufuatiliwa kila mara bila idhini yao.

Nini kifanyike kutatua changamoto hizi?
1. Mamlaka zitunge sheria kali dhidi ya udukuzi ama uharibifu wa mifumo ili kulinda mifumo, kudumisha uaminifu na ufanisi wa mifumo ya uchunguzi.
2. Mamlaka ziwe na miongozo iliyowazi ya kiasi cha kukusanya taarifa, kutambua athari zitokanazo na kukiuka faragha na kuweka hatua za kupunguza madhara iwapo ukiukwaji wa faragha utatokea.

Hitimisho
Ni ajabu jinsi teknolojia mpya kama kamera ya uchunguzi inaweza kutupatia faida lukuki za kiusalama na kimazingira katika miji yetu.
Zama zimebadilika, ni muda sasa wa mamlaka kama jeshi la polisi, halmashauri za majiji na miji na mahakama kubadilika na kuendana na teknolojia mpya kama kamera za uchunguzi ili kutatua changamoto za usalama barabarani, uhalifu na uchafuzi wa mazingira.
 
Upvote 1
Kamera za uchunguzi hufungwa nje ya majengo au kwenye nguzo za taa za barabarani urefu wa mita tatu mpaka tano. Manispaa, miji na majiji mengi ya Tanzania yamefanikiwa kufunga taa za barabarani zinazotumia nishati ya jua na hivyo kurahisisha uwekaji wa kamera zitazotumia nishati ya jua pia.
Simple tu tunaendeleza kwenye miundombinu iliyopo. Mfano pote penye taa pakiwa na kamera itakuwa ni hatua nzuri sana.

Kuwatia hofu madereva kutovunja sheria za usalama barabarani kwa kuamini wanaonwa na kamera.
😆😆😆😆😆 hii itafanya kazi hata kama mifumo imeharibika. Tunahitaji tu kuwaonesha mfano wakikamatika. Baadaye inakuwa ndo utamaduni. Neno 'kuna kamera' pale linatosha sana.

  • Kamera za uchunguzi zikiunganishwa na mifumo ya halmashauri za majiji zitawezesha halmashauri hizi kupata taarifa za maeneo yenye taka zinazohitaji kuondolewa kwa haraka. Hii itawezesha taka kuondolewa haraka tofauti na mifumo ya awali ya kupitisha magari ya kuzoa taka kwa ratiba.​
Tunaingia kwenye enzi ya smart cities

Matumizi ya kamera za uchunguzi huibua wasiwasi kuhusu ukiukaji wa faragha, kwani watu binafsi wanaweza kuhisi wasiwasi kufuatiliwa kila mara bila idhini yao.
Hili kwa kweli raia inabidi watambue kuwa kuna kitu kinaitwa social contract. Tunaachana na baadhi ya haki ili kupata faida ya pamoja kama jamii moja. Asiyetaka, basi ahamie vijijini au porini, wenzetu wanaita off-grid

Ahsante kwa insha murua
 
Simple tu tunaendeleza kwenye miundombinu iliyopo. Mfano pote penye taa pakiwa na kamera itakuwa ni hatua nzuri sana.


😆😆😆😆😆 hii itafanya kazi hata kama mifumo imeharibika. Tunahitaji tu kuwaonesha mfano wakikamatika. Baadaye inakuwa ndo utamaduni. Neno 'kuna kamera' pale linatosha sana.


Tunaingia kwenye enzi ya smart cities


Hili kwa kweli raia inabidi watambue kuwa kuna kitu kinaitwa social contract. Tunaachana na baadhi ya haki ili kupata faida ya pamoja kama jamii moja. Asiyetaka, basi ahamie vijijini au porini, wenzetu wanaita off-grid

Ahsante kwa insha murua
Shukran sana mkuu hakika zama zimebadilika.
 
Back
Top Bottom