SoC04 Tanzania yetu baada ya miaka 5

SoC04 Tanzania yetu baada ya miaka 5

Tanzania Tuitakayo competition threads

packs_310

New Member
Joined
Jun 19, 2024
Posts
1
Reaction score
0
SEKTA YA ELIMU TANZANIA BAADA YA MIAKA KUMI.

sekta ya elimu ni sekta muhimu sana katika ukuaji wa maendeleo katika taifa sababu ndiosekta pekee ambayo inazalisha wataalamu mbalimbali ambao wanategemewa katika sekta zingine kama vile sekta ya afya,viwanda,habari n.k hivyo basi kutokana na umuhimu wa sekta hii ya elimu nchini ninaiyona Tanzania baada ya miaka kumi ikiwa imepiga hatua kubwa ya maendeleo katika hii ya elimu kama serikali ikifanya mambo yafuatayo.

Jambo la kwanza serikali inapaswa kubadili mitaala ya elimu mfano mitaala iliyopo kwasasa katika elimu haitoshi kuandaa wataalamu wenye maarifa yakutosheleza ilikuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia kama nilivyo tangulia kusema hapo juu kuwa sekta ya elimu ndio sekta pekee ambayo inazalisha wataalamu ambao wanatumika katika maendeleo ya sekta nyingine mfano hivi sasa serikali inatenga bajeti kubwa sana kusomesha wataalamu mbalimbali nje ya nchi hii inaonyesha wazi kwamba mifumo ya elimu haikidhi mahitaji hivyo bas serikali inapaswa kutenga bajeti kubwa katika sekta ya elimu ili kuzalisha wataalamu wetu wenye maarifa yakutosha kama serikali ikifanya hivyo bas naiyona Tanzania kwa miaka kumi itakuwa Tanzania yenyemapinduzi makubwa yakimaendeleo kupitia sekta hii ya elimu.

jambo lapili serikali inapaswa kuanzisha shule nyingi zenyekutoa maarifa ya vitendo kwa wanafunzi kama ilivyo kwasasa VETA na SIDO serikali inapaswa kutenga fedha zakutosha katika kujenga vituo hivi vingi ilikuwezesha vijana na wanafunzi kwaujulma ilikuweza kupata stadi za kazi kwa vitendo ili kupata wataalamu wenye weledi mkubwa sambamba na hayo pia kupitia elimu hiyo ya vitendo ambayo vijana watakaiyo ipata itawapa fursa ya wao kujiajiri nakutokomeza umaskini kwakiasi fulani kwakufanya hivyo Tanzania baada ya miaka kumi itakuwa na maendeleo makubwa katika sekta ya elimu kwakuzalisha wataalamu wenyeuwezo mkubwa kiutendaji nakutokomeza wimbi la ukosefu wa ajira kwavijana kutokana elimu watakayoipata.

Jambo la tatu ninaiyona Tanzania yenyemaendeleo makubwa katika sekta ya elimu baada ya miaka kumi kama serikali ikitoa elimu bure kwa wanafunzi kwa ngazi zote za elimu yaani kwa wanafunzi wa viyo vikuu na kwawale wanafunzi wanaojifunza katika vituo vya elimu ya kivitendo yaani wanafunzi wa VETA na SIDO pia serikali inapaswa kuwakopesha fedha au nyenzo mbalimbali za kiutendaji yaani vifaa baada ya kuhitimu masomo yao hii itasaidia kupata mainjinia waliokamilika,mafundi na wataalamu mbalimbali ambao watakuwa na uwezo mkubwa wakiutendaji kwasasa hivi Tanzania imekuwa na wasomi wengi sana ambao wamepata elimu lakini elimu waliozo zipata haziendani na uhalisia wamazingira yaliyopo yaani elimu walizo nazo zinategemea zaidi kuajiriwa na sio kujiajiri.

Jambo la nne ni uzalishaji waalimu au wakufunzi wenye weledi na ubora;Tukianza na vijijni kumeakua na hamasa kubwa ya elimu ina maana kwa kila mzazi sasa anatamani mwanae aweze kupata elimu lakini kumekuwa na ukosefu wa waalimu au wakufunzi na hii inatokana na miundomu isiyo wezeshi na hii kupelekea walimu kukataa kufundsha shule za vijijini na hivo wanafunzi kukosa waalimu bora na wenye weledi hivyo bas serikali iweze kujenga vyuo vya bora vya ualimu kwa kila mkoa mfano mwalimu nyelele kwa dar es salaam hii itaweza kusaidia kupata waliimu wengi na walio bora kila mkoa na kuweza kupunguza hadha ya shule za vijijini kukosa waalimu.

Jambo la tano ni kupunguza kwa fedha za malipo ya ada kwa vyuo vya ufundi stadi;kwa sasa kuna vijana wengi sana mtaani wamekuwa wakilia kuwa kuna ukosefu wa ajira,wengne kushinda vijiweni na kujiingiza katika makundi ya kiharifu, hivyo bas serikali ijitahidi iweze kupunguza kama sio kuondoa ad kataka vyuo vya ufundi stadi ili vijana wengi waweze kupata elimu pamoja na ujuzi waweze kujikwamua katika janga hili la ukosefu wa ajira.

Jambo la sita uwezweshaji wa vijana kwa kukopeshwa pesa kwa ajili ya kujiendeleza kataka shughur mbali mbali; pale vijana watapo kuwa wameitimu masomo yao yao ufundi stadi waweze kukopeshwa fedha ama vifaa ambavyo vitaweza kuwasaidia kataka shughuri zao mbali mbali za kujipatia kopato ambapo watapangiwa mfumo maalumu wakuweza kulejesha deni kidogo kama ilivyo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu wanapokopeshwa fedha kwa kujiaendeleza na masomo na baadaye kuziljesha wakiwa makazini:

SECTA YA AFYA BAADA YA MIAKA KUMI
Secta ya afya pia ni miongoni mwa secta muhimu sana hasa kwa nhi yetu ya tanzania kwa sababu ili nhi iweze kuendlea inahitaji wananchi wenye akili imara nakikubwa zaidi ni afya njema;kwa sasa nhini kumekuwa na mdororo mkùbwa sana hasa katika secta ya afya na wanachi wengikufariki kwa mogonjwa aidha yale ya kuambukiza pia na yasio ya kuambukiza kwa kukosa kwa kukosa vituo vya afya au watalaam wa afya walio bora hvyo serikari inatakiwa ifanye mambo yafuatayo ili kudumisha secta ya afya nchini tanzania;

Jambo la kwanza: kujenga vituo vya afya kwa kila kata ama kijiji na na miundo mbinu thabiti kuwezesha ufikiaji wa vituo hvyo;kwa sasa kumekuwa na malalamiko mengi kwa wananchi hususa ni wavijijini kwa kukosa vituo vya afya vilivyo karibu na miundo mbinu kuwa mibovu yaani vituo vya afya kujengwa maeneo ya mijini tu na kufanya wananchi kutembea umbali mrefu ili kuweza kupata vituo vya afya na hili kupelekea wagonjwa kukosa matibabu na wakina mama wajawazito kuweza kujifungulia nyumbani na pia kujengwa miundo mbinu wezeshi kama barabara kwa magari ya msaada [ambulance) kuweza kuwafikia kwa wakati.

Jambo la pili kuongeza waudumu wa afya ikiwa ni madactari pamaja na manesi katika vituo vya afya kwa kila kata ama kijij nchini tanzania: kumekuwa na wimbi kubwa sana la ukosefu wa madactari katika hospitali zetu hasa zile za vijijini serikari iweze kuwajengea miundombinu wezeshi ili waweze kufanya kazi kwa weledi katika kila kituo cha afya husika.

Hitimisho, baada yakueleza mambo machache hapo juu ili Tanzania iweze kupiga hatua za kimaendeleo kupitia sekta hii ya elimu serikali lazima ijenge miundombinu wezeshi kwawanafunzi wakati wakujifunza yaani vifaa vyakujifunzia ili wanafunzi waweze kujifunza vitu kwa urahisi na uhalisia siokwailivyo hivi sasa.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom