Kati ya mambo yanayoikwamisha nchi yetu ya Tanzania kufikia maendeleo ya kimiundo mbinu pamoja na maendeleo hitajika ni udokozi yaani upigaji wa fedha za umma. Hii imesababisha baadhi ya miundombinu ishindwe kumalizika au kuishia njiani pamoja na hile inayomalizika kuwa chini ya kiwango kwa kuharibika ndani ya muda mfupi.
(Haya ni mambo matano yatakayotokomeza udokozi wa maliuma)
1. Kwa kudhibiti suala la nidhamu kuanzia ngazi ya familia.
“Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo” na siku zote “samaki mkunje angali mbichi”
Madili ya kukemea udokozi kwa kudokeza athari zake yakianza kumwingia mtoto akiwa bado na umri mdogo kimakuzi naona ni njia itakayoleta mabadiliko chanya pale maadili haya yatakapoambatana na mifano hai ya mataifa yanayoshindwa kuendelea kwa sababu za udokozi na kumdokeza yale yaliyodhibiti wizi wa mali za umma na kujipatia maendeleo, hii itamfanya mtoto achague fungu lililo jema nalo nila kuupinga udokozi wa aina yoyote na kwa njia yeyote.
2. Kwa kujenga na kuimarisha imani, yaani kujenga kizazi kilicho bora kiroho.
Kupitia taasisi zote za kidini watoto wafundishwe ni jinsi gani Mwenyezi Mungu aliyefanya kazi ya uumbaji wa mwanadamu na vitu vyote anavyochukizwa sana na ubadhirifu, mtoto aonyeshwe na kuambiwa mifano hai ya watawala na watendaji ambao walipokwa madaraka na nguvu waliyokuwanayo pale waliposhindwa kuenenda katika njia iliyonyoofu.
3. Kwa kuipa thamani fasihi inayobeba maonyo kama vile ushairi.
“Nina kisa cha rafiki yangu aliyekuwa akinidokeza kila mara kuwa yeye hawezi kuiba hata senti moja, nilipomdodosa kwa kina aliniambia kuwa alipokuwa mwanafunzi wa kidato cha tatu na cha nne yeye alisoma mashairi mawili, shairi moja la “moyo ishinde tamaa” na “taifa wamelizika” ambapo anadai haya ni mashairi yaliomkatakata mizizi yote ya udokozi wa fedha za hapo nyumbani kwao hadi na sasa kazini.
Sitaki niseme turudi kwenye fasihi ya kale kuwa fulani aliota nundu ya ng’ombe baada ya kuiba ng’ombe au fulani aligeuka jiwe kwa kuiba mali ya jirani yake fulani, fasihi ninayoongelea iseme wazi kuhusu wanawake wanaopoteza maisha kwa sababu ya kukosa dawa zinazoibwa hospitalini na ubovu wa miundombinu unaosababishwa na wapigaji pamoja na ugumu wa maisha unaowapata raia.
4. Kwa kwenda nyanjani
Watumishi kabla ya kuajiriwa au kupewa vitengo nyeti, wapelekwe kwenye maeneo yanayokosa huduma za kijamii au yanayopitia changamoto ngumu zinazo sababishwa na upotevu wa maliuma hususani “fedha” baada ya hapo wapewe jukumu la la kuleta mageuzi baada ya kuona adha na tabu zinazowapata wananchi “Aisifuye mvua umnyeshea” kwani ninachokisa mafunzo cha mtoto mwenye ndoto ya kusoma na kuwa hakimu kama si kuwa askari ili amwajibishe kisheria baba yake anayewakataza watoto wake kwenda shule ikiwemo na uonevu wa kijinsia kwa mama yake.
Pia pawepo na kipimo cha uadilifu na uchapakazi kwa manufaa ya taifa kwa watendaji/wafanyakazi.
Mfano: Wateuliwa wote wapewe kipimo cha utayari wa kuwatumikia wananchi sambamba na uadilifu. Unaweza kuweka mpango mkakati wa kumtuma kila mtendaji kwenda kwenye eneo gumu kimiundo mbinu kwa usiri au kificho watumwe watu au mtu wa kumpima mtumishi huyo kiutendaji kupitia utendaji unaoendana na uadilifu, wale watakao fuzu kipimo hiki wasomwe kiidadi pamoja na wale walioshindwa ili kuandaa kizazi chenye kutambua thamani ya uadilifu na uchapakazi kwani jambo hili litawakaa wengi akili na kujiweka tiyari katika utendaji kazi unao ambatana na uadilifu kama kigezo cha kuwa sehemu ya utendaji kazi “utumishi”.
5. Kwa kubainisha ukweli na uwazi
Uficho kuhusu manunuzi au matumizi ya fedha za umma yanashamirisha udokozi, lakini likiwa takwa la lazima kusoma mapato na matumizi, hii itazuia mianya ya udokozi kwenye miradi pale kila ya hatua ya utekelezaji itakaposomewa mapato na matumizi. Pia mtu mwenye taarifa za viashiria vya ubadhirifu wa fedha kwenye taasisi au mradi wowote apewe uwanja wa kuwasilisha taarifa alizonazo juu ya ubadhirifu unaofanyika ili vyombo vya uchunguzi vifanye kazi yake na vitakuwa vimerahisishiwa kazi hiyo kwa kupatiwa mwangaza au mwanzo mzuri wa kutekeleza majukumu yake.
Mwisho kabisa katika kutokomeza udokozi wa mali umma ni kuanzisha maadhimisho ya “SIKU YA UADILIFU TANZANIA” hii iwe siku au sikukuu mahususi kwa ajili ya watoto na katika maadhimisho haya, siku hii imtake kila mtoto afanye tendo lolote la kiuadilifu. Katika kuliongezea uzito jambo hili ningeomba kiongozi mmoja wa kitaifa ambaye ameisha tangulia mbele za haki hususani Rais, siku ya kifo chake kila mwaka hiwe ni sherehe au kumbukizi ya “Siku ya uadilifu Tanzania” hususani kiongozi yule mbaye dira yake kubwa ilikuwa ni kujenga maadili kwa watanzania. Kufanya hivi kutabadilisha mwenendo wa kila mbadhirifu kwani roho yake itamsuta kuona anashiriki au anaadhimisha siku ambayo yeye anaenda kinyume na matakwa ya siku hiyo. Siku hii iadhimishwe kuanzia kwenye ngazi ya familia, kata, mkoa hadi kitaifa.
MUHIMU: Uadilifu unaweza kukemea vitendo viovu kama vile rushwa na kufichua uozo unaotendeka katika jamii, sauti za viongozi mashujaa na wazalendo zinaweza kutumika kwenye maadhimisho ya sikukuu hii pale siku hii itakapo pata ridhaa na ikiangukia kwenye siku za masomo basi siku hiyo hotuba za wapinga ubadhirifu zitumike kufundishia watoto mashuleni kwa kurusha kipindi cha runinga au redio ndani ya kipindu cha dakika 40 za somo au zaidi, kufanya hivi kwa kila mwaka kutaleta chachu ya kila kijana katika kuona jambo hili linavyopewa kipaumbele nayeye ndiye anayelengwa kwenye mabadiliko chanya.
Tulijenge taifa la waadilifu kupitia malezi ya uadilifu sambamba na maadhimisho ya siku ya uadilifu tanzania huku tukisisitiza uchapakazi kwani uchapakazi bila uadilifu ni kazi bure sababu kile kitakachozalishwa kitawanufaisha wachache kwa kukiingiza mifukoni mwao bila kujali hatima ya watu wengine ambao ndio wengi. Ni imani yangu kuwa uadilifu ndio utakao tufikisha watanzania kwenye Asali tuliyohaidiwa kiinchi toka enzi na enzi.

Upvote
0