treblig.1979
New Member
- May 9, 2011
- 2
- 0
Yes hii ndio Tanzania tuliyoitaka, changamoto pande zote, mifumko ya bei, ugumu wa maisha, unaochangiwa pia na ungezeko la bei la hata huduma za jamii kama matibabu, maji, umeme ambao hata hivyo haupatikani na mengine mengi. Jamani huu ni wakati wa kuamka usingizini, na kila mmoja mahali alipo ajiulize atafanya nini ili kulikomboa taifa letu kutoka katika utumwa huu. Lazima kwanza tujione kuwa tupo utumwani, ndipo tuone sababu ya kujikomboa kwa njia za amani kabisa. Mwalimu alipotutangazia uhuru ambapo ndio tu tulitoka utumwani alisema " Tutapambana na maadui watatu, ujinga, njaa na maradhi, tujiulize maadui hawa bado wapo?, na kama wapo je hatupo utumwani bado? Mungu atusaidie na atupiganie watanzania na zaidi atuwezeshe kutoka katika katika hali hii.