Tanzanian actor Steven Kanumba reported dead

rip kanumba , umeacha pengo ktk sanaa
 
Wadau nimepata habari hivi punde TBC wametangaza kifo cha kanumba
 

Yule binti ndio alikuwa mwandani wake? Poleni sana wafiwa.
 
jamani mimi sio mpenzi wa bongo movie lkn kifo cha kanumba kimeniuma sana mwenye details za kifo chake atueleze please!
 
inaaminika kasukumwa na mpenz wake akaangukia kisogo. .
 
TAARIFA NILIZOZIPATA MPAKA SASA KUHUSU KIFO CHA MWIGIZAJI STEVEN KANUMBA.

Posted by Millard Ayo

Taarifa nilizozipata sasa hivi kutoka kwa mwigizaji Dino, ni kwamba kweli mwigizaji STEVEN KANUMBA amefariki dunia na inaaminika chanzo cha kifo chake ni baada ya kuanguka na kuanza kutoa mapovu hapohapo nyumbani kwake, alikua akiishi na mdogo wake anaitwa Fetty aliekua chumba kingine ambae amethibitisha kweli kwamba alimkuta kaka yake akiwa ameanguka.

Polisi wameondoka nyumbani kwa Kanumba muda mfupi uliopita baada ya kuwachukua waliokua wanaishi na Kanumba akiwemo mdogo wake Fetty ili kwenda kusaidia maelezo ya kilichotokea.

Bado watu wanazidi kuongezeka nyumbani kwa Kanumba ambapo tayari idadi kubwa ya wasanii wenzake wamefuka pamoja na
watu mbalimbali, millardayo.com itaendelea kukufahamisha kinachoendelea kadri taarifa zitakavyozidi kupatikana.

Ila kumekua na taarifa nyingine ambazo hazijathibitishwa kwamba Kanumba alianguka na kuumia kichwani baada ya mpenzi wake ambae anatajwa kuwa ni mwigizaji LULU kumsukuma na kuanguka wakati wanagombana.

‘Inasemekana' Kanumba wakati akijiandaa kutoka saa sita usiku aliingia bafuni kuoga, alipotoka alimkuta Lulu akiongea na mwanaume mwingine kwenye simu ndipo alipokasirika na ugomvi kuanza.

Alipelekwa hospitali Muhimbili ambako muda mfupi baadae alifariki dunia, mwili wake bado uko katika chumba cha kuhifadhia maiti Muhimbili hospital.
 
Duh Kanumba alikuwa anammega Lulu?Haya Lulu zamu yako kumfuata Kajara segerea.
 
R.I.P Kanumba U will be missed!!! mwenye picha ya LULU tuwekeeni tafadhali.
 
..........jamani, jamani!! Ni kweli Kanumba katutoka, nimeona wanatangaza asubuhi hii kwenye TV.
Ama kweli sisi ni maua, muda wowote tutasinyaa!! I have always loved your movies........I will surely miss U.
RIP Kanumba.
 
Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Kanumba. Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…