Hapo ndio nachoka mimi, pamoja na Chadema kuwa na mwanasheria mnayeseama kabobea lakini Chadema hiyo hiyo ilishindwa kutatua tatizo la Lema. kuna mahakama ngapi ambazo Lema anheweza kupeleka shauri la rufaa yake na akasikiliza, kuanzia mahakama kuu ya Tanzania, mahakama ya rufaa ya Tanzania, mahakam ya kikanda EACJ iliyoko Arusha, mahakama ya Umoja wa Afrika ambayo pia inakitenge hapo hapo Arusha. Unataka kusema mahakama zote hizo ziko mifukoni mwa serikali ya CCM?
Mimi sipingi wao kuwa Nairobi, lakini napinga upinzani wanatumia janga la Lissu kama fursa. Mara michango kitu, mara video za shutuma, mara Tanzania sio salama, mara udikteta. Hivi kweli chadema imeshindwakupata $50.000 huku inalamba ruzuku $1.2million? Mtu ana bima ya bure inayolipiwa na bunge, ingeweza kumpatia matibabu ya aina yoyote lakini wenzetu kidogo imekuwa fursa. Hata hiyo mnayoisema serikali ya Tanzania ni mbaya, mbona serikali ndio ililkuwa ya kwanza kutoa offer ya kumuhudumia Lissu lakini wakubwa Chadema wakapiga chini? Mtu hada damu hazijakauka hawooo ....wamemkibiza Nairobi kama sio fursa ni nini. Matibabu anayoyapata Lissu Nairobi naweza kukuhakikishia angeweza kuyapata hapahapa Dar. Mpaka leo hii, hakuna ushirikano toka kwa watu walio kuwa karibu na Lissu siku ya tukio kutu ambacho kinakwamisha juhudi za kujuwa ukweli uko wapi.
..ktk shauri la Godbless Lema CDM walifuata taratibu zote hizo ulizozieleza,lakini mahakama zilikuwa hazitoi haki. By the time wamevuka vikwazo vyote na kufika mahakama ya rufani Godbless Lema alikuwa ameshakaa gerezani miezi 5. Jaji wa Mahakama ya Rufani aliyemtendea haki Mh.Lema aliwalaani mawakili wa serikali kwa kuichafua mahakama kwa mapingamizi waliyokuwa wakiweka ili Mh.Lema asipewe dhamana.
..Kinachokwamisha CDM kupata haki siyo kuwa na wanasheria wabovu, bali baadhi ya mahakimu kuwa compromised na kutumiwa na serikali kukandamiza wapinzani. At least mahakama kuu na mahakama ya rufaa wapo Majaji wenye ujasiri wa kutenda haki, lakini by the time CDM wamekata rufani na kufika ngazi hizo za juu tayari wanachama wao wameshaumizwa, wamesumbuliwa, wamepotezewa muda, na wamepoteza fedha na rasilimali zao.
..Mpaka hivi tunavyozungumza TL ana kesi zaidi ya tano. Kesi ambazo naweza kusema zinatokana na mashinikizo ya kisiasa. Kesi hizo atakwenda kukabiliana nazo MUNGU akimponya. Vilevile wanachama wa CDM zaidi ya 300 wana kesi ktk maeneo mbalimbali ya Tz. TL alikuwa tegemeo lao kwasababu yeye ndiye mwanasheria mkuu wa chama.
..Suala la kwenda Nairobi inabidi ulielewe kwa mapana yake. Nadhani unapaswa kuzingatia hali ya wasiwasi juu ya usalama wa TL waliyokuwa nayo FAMILIA pamoja na uongozi wa CDM ikiwa mgonjwa angekuwa-refered kwenda Muhimbili. Kama wahusika walimpiga risasi mchana kweupe katika compound ambayo Naibu Spika na mawaziri wanaishi nini kingewazuia kumvamia huko Muhimbili? Hivi unafikiri hakuna uwezekano wa wauaji kuvaa kama madaktari na kumvamia tena TL wakiwa na bunduki za silencers and finish him off?
..Kwa hiyo suala la TL kupelekwa Nairobi lilitokana na security concerns more than anything else. Na pia unaposema serikali imetoa offer ya kumhudumia inabidi ujiulize offer hiyo ni ktk mazingira yapi?
..Kwa maoni yangu serikali[waziri wa afya, na katibu mkuu] na Spika Ndugai walikosea kulazimisha TL afuate taratibu wanazofuata wabunge wanapokuwa na matatizo ya kiafya. TL hakuwa na tatizo la kiafya bali alikuwa na DHARURA YA KIAFYA. Wahusika hao walitakiwa wafanye maamuzi ya haraka ya kuokoa maisha ya TL huku wakizingatia kuihakikishia familia yake usalama wa mpendwa wao.
..Zaidi mpaka sasa hivi sielewi kwanini serikali imekaa kimya kuanzia kutoa salamu za pole, na hata kuhakikisha kwamba TL anahamishiwa hospitali nyingine yenye specialized treatment kwa majeruhi wa silaha za kivita kama TL. Mimi naamini serikali inao uwezo wa kifedha, kinachokosekana ni nia ya kumsaidia TL. Kwanini serikali imeamua kuwasusia mgonjwa familia na CDM?
..Kama serikali ingetekeleza wajibu wake wa kumlinda TL tusingefika hapa tulipo. TL asingeshambuliwa na silaha za kivita mchana kweupe. Lakini zaidi, kama serikali ingeamua kumsadia matibabu TL basi hawa wana-CDM unaosema wanatumia tukio hili kama fursa wasingekuwa wanalaumu, au wasingepata "fursa."
NB:
..Kuna madai kwamba ndege iliyokuwa impeleke TL hospitali ya Muhimbili haikuwa ndege inayofaa na ingetumia muda mrefu kusafiri kuliko ndege iliyokodishwa na CDM kumpeleka TL Nairobi.
Huyo hapo juu ni Mh.Peter Lijualikali mbunge wa CDM Kilombero. Hapo alikuwa anaburutwa kupelekwa gerezani kutumikia kifungo cha miezi 6. Chama kilimkatia rufaa na kuweza kushinda lakini alishatumikia miezi kadhaa gerezani na kazi ngumu. Wakili aliyesimamia rufani hiyo ni Tundu Antipas Mughwai Lissu.
cc
MK254