Sanctus Mtsimbe
R I P
- Jul 14, 2008
- 1,820
- 1,032
- Thread starter
-
- #41
Sanctus Mtsimbe,
Mkuu wazo zuri sana lakini kitu kimoja tu.. Ulipoweka kiingilio, hii kidogo haikukaa sawa..
Ni muhimu sana kwa chombo kama hiki kujaribu kuvuta watu ktk mkutano wake wa kwanza hasa ikiwa unafanyika nyumbani Tz. Unapoweka kiingilio una limit nafasi na kuondoa uwezekano mkubwa wa kufanikisha kikao cha kwanza.
Ni wazo zuri sana kuunda Taasisi hii, lakini ikiwa serikali yenyewe haitambui umuhimu wa Taasisi hii sioni sabau kabisa ya kujaribu kuitongoza serikali. Taasisi zote za Diasporas huanzishwa kwa baraka za serikali zao na ukweli ni kwamba serikali nyingi hujaribu kuuza hoja hii kwa wakazi wake nje badala ya wakazi wa nje kujikusanya wao wakaanzisha chombo hiki ama kuishawishi serikali, jambo ambalo naliona hapa.
Na kulingana na mfumo mzima wa Utandawazi, hawa Diaspora ndio huwa importer wa asilimia kubwa ya mali zinzotoka nchini kwao..Hawa ndio mabalozi wa Uchumi wa nchi zao wakiuza bidhaa hadi culture yao. Leo hii hatuna sababu kabisa ya kupeleka Korosho zetu India ambao wana soko Marekani hali meneja wa masoko ktk shirika la Marekani ni Mtanzania...
Acha mbali kuwa na meneja, wapo Watanzania wanafahamu mashirka yanayo agiza Korosho toka India. Hatuan sababu kabisa ya mali yetu kupitia India ili ipate soko Marekani..Huo ulikuwa wakati wa vita baridi..Ukuta wa Berlin kiuchumi umeisha vunjwa wazee wetu..
Leo hii wapo Watyanzaniua wenye madini husafiri hadi Thaioland na China kuuza vito vyao kwa walanguzi China hali tunao Watanzania wanaoweza kuifanya kazi hiyo na kwa malipo mara mbili..Mbali na hayo, masomo ya juu ktk University na kadhalika ni vyama hivi huwawezesha wananchi wake kupata nafasi nchi za nje kirahisi zaidi na kwa gharama ndogo ktk exchange programs acha mbali Matibabu ktk Hospital na Zahanati..
Wakati umefika serikali yetu ikome zile fikra za Kijamaa na kikorosho..Diasporas ni win win situation, kwa msemo wa Kikwete!
Mkuu nitakuwepo ktk mkutano, nikijaliwa - Inshaallah!
Ijumaa nishai
bora wangefanya Jumamosi...asubuhi mnaenda kwenye mkutano mpaka time ya Lunch kisha mchana haoooo mnarudi kubadilisha nguo kwa ajili ya kwenda kwenye shughuli zingine
Ijumaa kama unavyojua Dar na ile foleni nani atakuwa na muda wa kwenda kwenye mambo ya diaspora?
Pili kwa nini wasingechukua ule ukumbi wa BOT au pale Movenpick?
Hii kitu is bound to fail...hivi kuna mtu anayo website yao?
Hii mada yenu (TPN) inachekesha sana:
Mada: Namna Wanataaluma Wanavyoweza Kuchochea Maendeleo
.....and that's it!
Watakaochangia mada mtawaorodhesha lini?
Wakihudhuria watu 300, makusanyo ni 15,000,000. Where does this money go?
SOURCE: http://issamichuzi.blogspot.com/2009/11/kongamano-la-wanataaluma-waishio-ndani.html#comments
Waandaaji: TPN Costech - TSN OUT UDSM - Serikali
Santu
Mimi nitakuja [inshallah]; ila uwe wazi kwamba 50K is way high kwa huduma za tulip labda kama mnataka kulipata posho kama akina mwakyembe
Nitakuja na naomba kama unaweza nitumie concept paper
Tanzania Professionals Network (TPN)
Nyumbani Ni Nyumbani 2009
Kongamano la Wanataaluma Waishio Ndani na Nje ya Nchi
Mada: Namna Wanataaluma Wanavyoweza Kuchochea Maendeleo
1.Namna gani Wataalamu Wanavyoweza Kusaidia Kuweka Vipaumbele vya Kitaifa katika Kujenga Uchumi Imara
2.Ni Vipi Wanataaluma Wanaweza Kusaidia Watanzania wa Kawaida Waweze Kushiriki Katika Ujenzi wa Uchumi wa Taifa na Kuboresha Maisha Yao
3.Jinsi Wanataaluma Wanavyoweza Kukabiliana na Changamoto katika Kuleta Maendeleo ya Kiuchumi, Kisiasa, Kielimu, Kijamii, nk.
4.Namna Gani Wanataaluma Waliopo Nje ya Nchi Wanaweza Kushiriki Kuleta Maendeleo Nchini
5.Wanataaluma na Dira ya Maendeleo ya Taifa Letu: Tukotoka; Tulipo, Tunakokwenda: Changamoto na Ufumbuzi Wake
6.Je, Ni Wakati Gani Mwafaka Wanataaluma Walazimike Kuchukuka Hatua Za Kuleta Mabadiliko Na kwa Namna Gani?
7.Ni Mikakati Gani Watumie Wanataaluma Kupeana Habari na Taarifa Za Uhakika na kwa Muda Muafaka/
Siku na Muda:
Ijumaa; 18th December 2009; Saa 2.00 Asubuhi -11.00 Jioni
Mahali:
Golden Tulip Toure Drive, Msasani Peninsula
Washiriki:
Wanataaluma na Wasomi Wote Wazalendo Mnaombwa Kufika Bila Kukosa
Ada ya Ushiriki:
TZS 50,000 (Kwa ajili ya Ukumbi; Chakula; Tea na Snacks, PA, Documents nk)
Angalizo:
Viongozi wa Vyama Vya Kitaaluma na Wanataaluma Wanaharakati wa Maendeleo Walioko Mikoani Wamewekewa Nafasi Zao na Watalipiwa Ada ya Ushiriki; Tuwasiliane. Huu si wakati wa Kulaumu. Kama Umeguswa naMada, usikose kuja Kutoa Mawazo yako.
Waandaaji: TPN Costech - TSN OUT UDSM - Serikali
Mkuu Sanctus.........vipi kuhusu live communications na kwenye mkutano.......be it video conference facility, radio or whatever the case may be....unauja tena teknolojia.........haya mambo yanawezekana.....kama hilo halipo basi mlifikirie kwa mikutano ijayo..........