Tanzia: Fauzia Abdallah mwimbaji mkongwe wa taarab afariki dunia

dubu

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2011
Posts
3,502
Reaction score
3,483


Mwimbaji gwiji wa muziki wa TAARAB asilia kutoka Zanzibar wa kundi maarufu duniani lenye miaka zaidi ya 105 Nadii Ikhwaan Safaa (Malindi Musical Club), Bi Fauzia Abdallah, amefariki dunia hospitali ya Muhimbili alfajiri ya Mei 11.

Bi Fauzia alitamba sana katika miaka ya 1980 akiwa na kundi hilo la Malindi Musical Taraab na nyimbo zake nyingi "Lishalo Limekwisha" na “Nimesalitika”.

Pia bi Fauzia alikuwa mke wa mtunzi mahiri na mpiga qanoun Ally Salum Bassallama wa kundi hilo maarufu ambalo ndilo kundi la mwanzo la taarab barani Afrika lililoanzishwa mwaka 1905 huko Zanzibar.

Bi Fauzia amefariki katika wodi ya Kibasila alikokuwa akipata matibabu ya saratani.

Marehemu ya Bi Fauzi ambaye ameacha watoto watatu, mazishi yamefanyika huko Zanzibar.

Mola amlaze mahala pema peponi amen.
 
Pole ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki ..

Pumzika Salama ..
 

Huu mziki watu wameutoa mbali na wanakufa na umasikini wao..hao walikua wanaimba kwa kuupenda mziki na si umaarufu..ajabu watoto wanatoka tandale wanaenda studio nakuimba maneno mawili tu NIMPENDE NANI wana make money dah!..huku manguli walioufikisha mziki hapo wanakufa kibasila
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…