TANZIA TANZIA: Getrude Rwakatare, Mbunge na Mchungaji wa Kanisa la TAG (Mlima wa Moto - Mikocheni B) nchini Tanzania, afariki dunia

Hivi Kanisa wanaposalia eneo Ni la familia au Ni la taasisi.Najiuliza Kama wanawe wakiamua kupauza na mnununuzi akabadili kabisa matumizi ya eneo sijui itakuaje kwa wafuasi wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  1. Kila mwanadam aliye zaliwa na mwanamke anasiku chache za kuishi duniani nazo zimejatabu na mateso pumzika kwa amani mama yetu kipenzi 😭😭😭😭
 
Leo sijui ni kwanini nimetokea Kukumbuka sana Maneno ya Wahenga hasa huu Msemo usemao Malipo ni hapa hapa Duniani.
 
Kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani Bungeni Mh Freeman Mbowe ameeleza kushtushwa kwake na kifo cha mbunge mwenzao mama Getrude Rwakatare.

Akiongea na waandishi wa habari katika viwanja vya bunge Mbowe amemtaja mama Rwakatare kama mtu makini aliyekubalika katika huduma zote alizoshiriki ikiwemo Bungeni, Kanisani na katika sekta ya watoa huduma ya elimu.

KUB Mbowe ametuma salamu za pole kwa Chama Cha Mapinduzi, Kanisa la Mikocheni Assemblies of God na kwa familia ya mama Rwakatare.

RIP mama Rwakatare

Source: Ayo TV

Maendeleo hayana vyama!
 
Nimecheka hiyo ya kugombania remote, ndio ukweli kila mtu anataka aangalie kinachomuhusu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitu siwezi sahau Ni pale nilipoona Mchungaji Rwakatale anashangilia kwa nguvu na kugonga dawati bungeni kufurahia kauli ya Mh. Bulembo kwamba "Zitto Kabwe auawe eti ni msaliti!!!" Siasa hizi Ni Kama pombe, Kuna wanaokunywa akili zikachangamka zaidi positively, Ila Kuna wanaokunywa wanapoteza akili kabisa" Mtumishi gani anafurahia kauli ya mtu kuuawa hata Kama amekosa??! Nilitegemea aombe angalau dakika 3 kwa Speaker ili amuombee Zitto kwa mungu ambadilishe. RIP Rev. Dr. Getrude Rwakatale. Sote wa Mungu na njia Ni moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukishakuwa maiti utapewa sifa zote nzuri hata kama sifa zingine hustahili kupewa utapewa ila Mungu ndio atakayejua hatima ya maisha yetu baada ya kifo. Mungu akutendee kulingana na matendo yako uliyotenda hapa dunia. R.I.P mama Lwakatare

DUMU KUBWA
 
"Mbele ya kifo hautambi" 😷 credit Dr. Remmy Ongala
 
Naona umepanick mkuu [emoji23][emoji23]

Upepo wa kisuri suri na ukufunike jioni ya leo [emoji28]
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…