Tanzia: Kiungo wa Kagera Sugar, Behewa Sembwana afariki dunia

Queen V

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2012
Posts
775
Reaction score
1,332
Kiungo wa Kagera Sugar, Behewa Sembwana amefariki dunia leo alfajiri kutokana na kuugua tumbo.

Kiungo huyo amesumbuliwa na maumivu ya tumbo kwa muda mrefu, hali ambayo ilimlazimu kufanyiwa operesheni takribani mara mbili.

Nahodha wa timu hiyo, George Kavila amethibitisha kuwa Behewa amefariki baada ya kusumbuliwa na maumivu ya tumbo ambayo alianza kulalamika tangu wakiwa pamoja kikosini.

“Nakumbuka alianza kuumwa wakati tunacheza na Mwadui, alishindwa kutoka na sisi kwenda kule Complex baada ya hapo alipelekwa hospitali alipatiwa matibabu, lakini baadaye alihamishiwa Muhimbili ndio mauti yakamkuta akiwa hapo,” alisema Kavila.

Aliongeza kwamba mchezaji huyo ameondoka akiwa na umri mdogo licha na alikuwa amebarikiwa kipaji hasa katika kuuchezea mpira anapokuwa yupo uwanjani.
 
Wafiwa wanatangaza wamefiwa mtu ana like.
Tanzia nayo inakuwa liked na swali la kijinga!!
Kweli mazuzu wengi.
 
Alale pema marehemu...amiin!

George kavila 'babu' bado anacheza ... hongera zake, huyu jamaa wampe hata tuzo !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…