TANZIA: Kiungo wa zamani wa Azam, Jeba afariki dunia.

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
Dar es Salaam .Kiungo wa zamani wa Mtibwa Sugar, Azam FC, Ibrahim Rajab 'Jeba' amefariki leo jioni na anatarajiwa kuzikwa kesho kijijini kwao Ndijani, Zanzibar saa saba mchana.
Taarifa zilizothibishwa na Mkurugenzi wa Ufundi wa timu ya Chuoni ya Zanzibar ambayo ndiyo klabu ya mwisho kwa marehemu kuichezea Yusuf Mohamed amesema Jeba amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Mohamed alisema Jeba (27) tangu kuanza kwa msimu ambao tayari wamecheza mechi mbili za Ligi hakufanikiwa kucheza mechi yoyote kutokana na maradhi yake.
Kiongozi huyo alisema changamoto kubwa imekuwa marehemu hakuwa tayari kuweka wazi maradhi yanayomsumbua akisema ni siri yake.
Ingawa imekuwa ni siri, lakini taarifa ambazo hazijathibitishwa kutoka Zanzibar zinadai Jeba alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya ini ambayo yalikuwa yakimsumbua.
Aidha Mohamed alisema Jeba alilazimika kusimama kwa muda wa wiki mbili kufuatia hali yake kutokuwa sawa ambapo msimu huu alikuwa akimalizia mkataba wake na klabu hiyo.
Jeba alikuwa mmoja wa viungo bora nchini ambapo alivuma akiwa na Azam na Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Wakati akiwa Azam aliwahi kufanyiwa vipimo na kugundulika kuwa na maradhi ya moyo na kushauriwa kupumzika, lakini hakukubali akikanusha maradhi hayo.
Hata hivyo Azam ililazimika kuachana naye kutokana na ushauri wa madaktari na vipimo kuonyesha anahitajika kupumzika kwa muda mrefu.
Baadaye aliendelea kuzichezea klabu mbalimbali ikiwemo Mtibwa na kisha kurejea klabu ya Chuoni ambayo aliitumikia kwa muda mrefu.


Credit: mwanaspoti
 
RIP,nakukumbuka ulivyoewang'arisha akina mzamiru,Mo ibrahm na kichuya pale mtibwa
 
Inawezekana Azam waliona tatizo la zaidi ya moyo ndio maana wakamtosa
 
Pumzika kwa Amani Ibrahim Rajab Jeba, Mbele yako Nyuma yetu
 
Moja ya kiungo bora kabisa na mwenye nguvu kuwahi kumuona alipokua akiichezea Mtibwa sugar. RIP
 
Mbona hukusema kipindi yupo hai

Basi ngoja niwajumuishe na hawa wengine mapema wakiwa hai! Amri Kiemba, Nurdin Bakary, Athuman Idd Chuji, Hassan Dilunga, Mudathir Yahaya Abbas, Salum Abubakary, Mohamed Banka, Mzamiru Yassin, Jonas Mkude, nk.
 
Basi ngoja niwajumuishe na hawa wengine mapema wakiwa hai! Amri Kiemba, Nurdin Bakary, Athuman Idd Chuji, Hassan Dilunga, Mudathir Yahaya Abbas, Salum Abubakary, Mohamed Banka, Mzamiru Yassin, Jonas Mkude, nk.
Waanzishie Uzi kabisa ili kumbukumbu ibaki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…