Tanzia: LiverpoolFC afiwa na mwanae

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2010
Posts
8,169
Reaction score
3,351
WanaJF,

Napenda kuchukua fursa hii kuwajuza kuwa mwanaJF mwenzetu aitwaye LiverpoolFC amefiwa na mwanae mchanga leo asubuhi muda wa saa tatu na nusu katika hospitali ya Mount Meru iliyo jijini Arusha.
Taarifa ilichelewa kitufikia kidogo lakini naomba wote kwa ujumla wetu kuelewa juu ya tukio la huzuni lililomkumba mwenzetu.

Mazishi yameshafanyika leo tarehe 13.12.2011.

LiverpoolFC binafsi nakupa pole mkuu, nakuomba uwe mvulivu na mtulivu katika kipindi hiki kigumu sana ulichonacho. Zidi kumuomba Mungu, zidi kumtukuza Bwana maana sote ni wake. Narudia tena pole sana mkuu.
 
pole sana ndugu yetu Mungu akupe nguvu katika hiki kipindi kigumu
 
Inna Lillahi Wa-Inna Illaihir Rajiuun!!
Bwana alitoa, Bwana ametwaa, Mapenzi ya Bwana yatimizwe.
 
Pole sana.MUNGU AKUPE NGUVU katika kipindi hiki kigumu.
 
Pole sana ndugu yetu, Mungu akutie nguvu ktk kipindi hiki kigumu.
Tupo pamoja mkuu. Hiyo ni kazi ya Mwenyewe aliyekupatia ameamua kumtumia kiumbe wake kwa jinsi alivoona inafaa.
Jina lake lihimidiwe.
Amen.
 
Inna Lillahi Wa-Inna Illaihir Rajiuun!!
Bwana alitoa, Bwana ametwaa, Mapenzi ya Bwana yatimizwe.

Shark Allah S.W anasema kifo kinatosha kuwa waadhi kwa binadamu mkuu,
 
Pole sana ndugu yangu LiverpoolFC Mungu akutie nguvu ya uvumilivu kwa wakati huu mgumu wa uzuni, narudia tena pole saana wewe na mama mzazi wa mtoto!!!!!!!!!!

 
pole sana ndugu yangu. Mungu akutie nguvu na ampumzishe marehemu mahali pema peponi.
 
pole sana Mkuu wangu. Mungu akupe nguvu katika kipindi hiki kigumu na ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Mia
 
Pole sana sana mkuu
Mwenyezi Mungu akupe nguvu kukivuka kipindi hiki kigumu.
Pole sana mkuu na mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
 
Pole sana ndugu yangu LiverpoolFC Mungu akutie nguvu ya uvumilivu kwa wakati huu mgumu wa uzuni, narudia tena pole saana wewe na mama mzazi wa mtoto!!!!!!!!!!


Mtumishi wetu hakina umesema vizuri, kweli wengi tumempa pole LiverpoolFC lakini tumemsahau mkewe ambaye amepata machungu mara mbili;
1.0 Alijifungua kwa oparation
2.0 Kumpoteza mtoto.
Kiukweli pole sana LiverpoolFC pamoja na familia yako.
 
Inna li Llahi wa Inna iLlahi Rajiun.

Kila msiba wa kifo huwa ni mawaidha kwa tulio hai. Hakuna umri, si ujana si uzee, si mtoto si mkubwa, kifo kinaweza kumjia yoyote wakati wowote, tuhimizane kutenda mema.
 
Pole sana LiverpoolFc na wote.
Nakuombea ujasiri kipindi hiki kigumu.

Ni kazi ya Mola
 
Dada FF hakika umesema vizuri kabisa, sina la kuongeza.
Inna li Llahi wa Inna iLlahi Rajiun.

Kila msiba wa kifo huwa ni mawaidha kwa tulio hai. Hakuna umri, si ujana si uzee, si mtoto si mkubwa, kifo kinaweza kumjia yoyote wakati wowote, tuhimizane kutenda mema.
 
Pole sana Mzee wa Liverpool.
Mungu akutie nguvu
OTIS
 
Pole sana Mkuu LiverpoolFC pamoja na familia kwa ujumla. Mwenyezi Mungu akupeni moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…