Mama mzazi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Publishers, mtunzi mahiri wa hadithi, mjasiriamali na motivational speaker, Eric Shigongo, Asteria Kapela amefariki dunia alfajiri ya Ijumaa, Julai 27, 2018 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Kitengo cha Jakaya Kikwete alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.
Msiba upo nyumbani kwa marehemu, Mikocheni B jijini Dar es Salaam ambako taratibu za msiba zitafanyika.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.
Pole Shigongo na familia yako na Mungu akupe nguvu katika kipindi hiki kigumu.