TANZIA: Mama mzazi wa Zarina Hassan(Zari the Bosslady) afariki dunia

PRINCE PRIS

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2015
Posts
347
Reaction score
587

=====
Alhamisi iliyopita kulienea taarifa za hali ya ugonjwa ya mama huyo kutokuwa nzuri baada ya kudaiwa kupumulia mashine ya oksijeni kwenye Kitengo cha Wagonjwa Mahututi (ICU) katika Hospitali ya Nakasero iliyopo nchini Uganda akisumbuliwa na maradhi ya moyo na figo ambayo yamekuwa yakimsumbua tangu kufariki kwa mkwe wake, Ivan Ssemwanga.

Kwa mujibu wa chanzo ndani ya familia hiyo, mama Zari alipata matatizo ya moyo na figo baada ya kuanguka ghafla na kichwa chake kujigonga, hali iliyosababisha akimbizwe hospitalini haraka.
 
Kuna wakati ukisikia dunia nzito kwa kilo zisizojulikana basi ndio wakati kama huu anaoupitia Zari, hajamaliza machungu ya kufiwa na baba wa watoto wake anakutana na hili la kufiwa na mama yake mzazi. Pole sana Zarinah Hassan na familia yako kwa ujumla. Mwenyezi Mungu Mungu awape nguvu kuhimili haya mapito.
 
Mungu awape moyo wa subira, na mama upumzike pema, dah! inasikitisha sana misiba miwili muhimu kwako inatokea mfululizo, Mungu akupe subira Zari...
 
Na wote ni watu wa muhimu kwake, alisema mama yao aliwalea akiwa single parent. Watoto wamefiwa na baba hakuna hata aliyefikixha 18yrs
 
Du Bonge la Pigo kwa Zari.. Kaondokewa na Ivan Mpenzi wake wa Moyoni na Ameondokewa na Mama Mzazi Duu... Kwa kweli Mungu Amtie Nguvu sana huyu Mdada aisyekuwa na Makuu.. Ila Dimond has to Change sasa awe Mwanaume atoke kwenye Uvulana ili ajue jinsi ya Kuishi Kama Mwanaume na siyo Kuendelea Kuishi Kama Mvulana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…