TANZIA: Mwanamuziki mkongwe aliyeimba wimbo wa Lunch Time, Gabriel Agoya Omolo afariki dunia

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Mwanamuziki mkongwe na maarufu Afrika Mashariki na Kati ambaye alikuwa anatokea nchini Kenya Gabriel Agoya Omolo anayejulikana kwa wimbo wake maridhawa wa ‘Lunchtime’ wimbo ulioimbwa mwaka 1970 amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80.




Nyimbo yake


Amefariki akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Busia nchini Kenya baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Taarifa za kifo cha Gabriel Omolo zimetolewa na mke wake Alice Adeya jana January 3, 2018 akimwambia rafiki wa mume wake Charles Makawita ambaye nae alizaliwa na Gabriel Omolo katika kijiji cha Nyabeda.

“Mke wake aliniita jioni ya jana niende hospitalini, baada ya kugundua hali mumewe inazidi kuwa mbaya”- amesema Charles Makawita

Kulingana na gazeti la Daily Nation, Omolo ni mzaliwa wa kijiji cha Nyabeda eneo la Ugunja, Jimbo la Siaya ambako alilelewa pamoja na rafiki yake Makawita.

Omolo alikuwa na uwezo mzuri wa uimbaji kwenye bendi ya Equator Sound miaka ya 1960s alikoshirikiana na Daudi Kabaka, Fadhili William na Nshil Pichen, raia wa Zambia na Peter Tsoti.

Omolo ni mwanamuziki pekee kutoka Kenya aliyewahi kushinda tuzo ya kimataifa ya International Golden Disc mara mbili mwaka 1974 na 1976 kwa wimbo wake wa ‘Lunch time’

Alikuwa mwanachama wa bendi za Eagle Blue Shades na Komesha.

Chanzo: Millard Ayo
 
Rip.
Wkt wako uliutumia vema.
 
Aiseee wimbo wa lunch time kiukweli hauchoshi kuusikiliza sikuwah kumfaham na wala kulifaham jina la mwimbaj.
Alale mahali anapostahili
 
Huu wimbo niliwah kuukariri kipindi nimemaliza shule nafanya kazi kwa kujitolea, ikifika lunch bosi wangu anaagiza menu heavy mimi natoa macho tu, kuna kipande anaimba kuna wengine wanalala viwanjani wakati wenzao wanapata supu ya ngombe, hiki kipande kilikua kinanigusa saana kwakua ilikua ndo maisha yangu.
R.I.P Omolo
 
 
Huu wimbo naufahamu siku nyingi sana na muda wote nilifikiri umetungwa na kuimbwa na mwanamuziki wa tanzania! Kumbe mtunzi na mwimbaji ni mtu toka kenya - Gabriel Omolo? R.I.P Omolo, uliimba Lunchtime sisi sasa tunakuimbia Heaventime!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…