TANZIA: Mwanasoka wa zamani Zuberi Magoha afariki dunia

Rohombaya

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2011
Posts
13,067
Reaction score
10,393
Ni mchezaji machachari aliyewahi kuichezea timu mbalimbali ikiwemo klabu ya Simba.

Amefariki leo msiba uko nyumbani Yombo.

RIP striker
 
Inna Lillahi wa Inna illaihi Raji'un. Mungu akulaze mahala peponi mchezaji. Nakumbuka enzi hizo alihama kutoka Arusha (Ndovu) akahamia Simba enzi za King Mputa.
 
Malota soma , zamoyoni mogella, zuberi magoha, Ramadhani Lenny, Sunday Juma, Moses mkandawile, daud salum, Tobias makoma, Taliban hillal, Ezekiel Grayson juju man, na mtemi Ramadhani. Hii ndo ilikuwa first eleven. Magoha namba 10.
 
Mkuu umemsahau Mohamed Kajole Machela!.
 
Poleni wafiwa kwa msiba. Pumzika kwa amani, Zuberi Magoha. Ni yeye na Emmanuel Tenende ndio walioweka historia uwanja wa zamani wa Taifa, walipigana " kibambi" na mpira kupasuka, haijawahi kutokea tena hapo Taifa. Mechi ilikuwa kati ya Simba na Nyota Nyekundu. Wote walikuwa wanacheza namba Tisa na walikuwa wameshiba kweli kweli. Mmoja alikuwa analinda goli na mwingine anashambulia
 
Malota soma , zamoyoni mogella, zuberi magoha, Ramadhani Lenny, Sunday Juma, Moses mkandawile, daud salum, Tobias makoma, Taliban hillal, Ezekiel Grayson juju man, na mtemi Ramadhani. Hii ndo ilikuwa first eleven. Magoha namba 10.

daah rip zuber magoha,jamaa alikuwa anapiga mashuti makali saana, nafikiri kuna wengine kama mohd nyauba, abbas kuka,twaha hamidu etc,umewasahau
 
Huyu mtu anakumbukwa vizuri kwenye kikosi cha Simba kilichoipiga Al Ahly (National) pale kirumba 2-1 kwa magoli ya Zamoyoni Mogella na Mtemi Ramadhani. Kikosi kilikuwa na Mose Mkandawile, Musa Kihwelo "super", Talib Hilal, Thobias Nkoma, Athuman Maulid "big man", Ramadhani Lenny "Abega", Sunday Juma, Mtemi Ramadhan, Zuberi Magowa, Zamoyoni Mogella "golden boy" na Malota Soma "ball juggler". Al ahly ilikuwa na majina makubwa kama Rabia Yassin, Magdi Abdelghani, Mohamed El Khatib "bibo" na wengineo. Ilikuwa hatariiiii!!! RIP Magowa.
 
daah kaka kweli wewe mtu wa mpira,umenikumbusha rabii yassin , beki matata saana, RIP magoha, i love SSC
 
Nimehuzunishwa kwa kifo cha ndg. Zuberi Magoha. Hakuna jinsi, sisi ni mavuno shambani mwa bwana.
RIP Zuberi Magoha.
 
Hii ni huzuni kwa wapenda kandanda wote wa Tanzania na si Simba SC pekee...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…