Tanzia ya Dkt. Dau kwa rafiki yake hayati Benjamin William Mkapa

Ni
Enzi za Dau,ili upate kazi nssf,kwanza uwe wa imani yake.....mengine yanafuata.
Ni kweli Kuna jamaa yangu yupo NSSF Morogoro aliwahi kunithibitishia hilo,Tena akaenda mbali zaidi akasema " Huku kwetu Nssf Kuna udini hataree,kupita hata idara ya utumishi chini ya Hawa Gassia" nakumbuka ilikuwa kipindi Cha awamu ya nne
 
Alichofanyiwa Dau, ni hichohicho wanafanyiwa watu wengi kwa makusudi ili wasipate mafanikio au kazi pale wapinzani wanapoona jua la wenzao linachomoza. Hii inafanana na wale madaktari wa Mbeya waliochafuliwa kupokea rushwa ya ngono, kitu kilichokuwa staged kabisa na mpinzani mmoja aliyekuwa akim target mmoja wa madaktari.
 
Hongera Dr Ramadhani Dau kwa kumtendea haki Mzee Mkapa.

Kiukweli hata mimi ni mkristo tena Mkristo sana niliyelelewa sehemu ya Wakristo Peramio. Ila nachukizwa sana na tabia ya wakristo wenzangu kuwaelewa au kuwachukulia vibaya waislamu ambao wamejikita sana kwenye dini yao.

Simkubali Mzee Mkapa kwenye mengi sana ila kwenye yote na mimi lazima niseme ukweli kuwa Mzee Mkapa hakuwa mtu wa majungu na kwake fitna ilikuwa kweli mwiko.

Kwake haikuwa shida kama mtu kaweka msikiti au kanisa ofisini as long as huyo mtu anadeliver kwenye utendaji wake. kwenye haya mkapa alikuwa sahihi sana.
 

Asante sana kaka

Mtu ukiwa Muislamu na unaipenda dini yako na unaiishi, kuna watu wanachukia sana

Lakini Makonda akienda kanisani akasema nchi hii iko chini ya kanisa, wala huoni wakishtuka na kumuita mdini. Hii ni kwa sababu kwao Maisha ni katika lenzi ya Ukiristo tu na kwamba life inapaswa iwe hivyo, na si vinginevyo. Ukifanya vinginevyo basi wewe ni mdini.

Kwa watu hawa, Ofisi za serikali zikipambwa miti ya Krismasi kipindi cha msimu wa Krismasi siyo tatizo, Ila Muislamu akisali ndani ya ofisi yake muda wa break ya lunch kwake hilo ni tatizo kubwa.

Kwa watu hawa mtu akiweka muziki wa kwaya kwenye computer yake huku akijifanyia kazi yake ndani ya ofisi ya serikali kwao siyo tatizo lakini muislamu akivuta tasbihi, tayari nongwa, maneno kila aina hadi kwa mabosi kuwa fulani ni Mujahidina.

Hapa Dau kamzungumzia mzee Mkapa kama mtu ambaye alikuwa fair, Mtu ambaye hakuwa mdini.

Dau Kazungumzia jinsi Mkapa alivyowapa Waislamu majengo ya TANESCO Morogoro wajenge chuo chao kikuu. Huu ni wema na legacy iliyoje!.

Mkapa alikuwa fair sana na ndiyo maana, akachukua na Majengo ya iliyokuwa benki ya NBC iringa akawapa wakatoliki wajenge chuo cha Ruaha Catholic University

Akatoa Majengo ya iliyokuwa Mazengo Secondary akawapa Waanglican nao wakajenga chuo chao kikuu huko Dodoma

Na akatoa majengo ya Magamba Secondary akawapa Walutheri nao wakajenga chuo kikuu

Huyo ndo Mkapa, Kiongozi bora na fair kabisa.
 
Hizi Sifa zote za Dkt. Dau alikuwa anasubiri Kwanza Rais Mstaafu Mkapa arudishe Namba yake Mbinguni ndipo aje atudanganye na ajifarague hivi?
Sio Dr Dau tu, wote ndio wamefanya hivyo na ndivyo tulivyo tunasubiri ukifa tutakusifia sana. Hata bwana mkubwa alikuwa anasema nchi imechezewa sana, imeliwa, wastaafu wanawashwa n.k lakini leo anasifia.
 
Mazengo ilikuwa mali ya Anglikana kabla ya kutaifishwa na serikali enzi za ujamaa.Hao hawakupewa bali walirudishiwa mali yao.Hii Ni sawa na Forodhan alias St. Joseph kwa wakatoliki au Mkulima Stein wa ndege kule south .
 
Mazengo ilikuwa mali ya Anglikana kabla ya kutaifishwa na serikali enzi za ujamaa.Hao hawakupewa bali walirudishiwa mali yao.Hii Ni sawa na Forodhan alias St. Joseph kwa wakatoliki au Mkulima Stein wa ndege kule south .

OK thanks kwa ufafanuzi.
Magamba secondary je?
 
Ni kipi kipimo cha kudeliver ambacho kinahalalisha kuvunja taratibu za kazi? Kila mfanyakazi akisema atumie resource za muajili kujenga sehemu ya ibada si itakuwa chaos.
 
Ni tatizo kubwa sana kwa kweli. Nikiri wazi kuwa waislamu wanaoishi dini yao wamekuwa wana pata madhira sana kwenye maisha yao. Na huu ni ujinga na ubaguzi kama ilivyo kwenye mengine.

Mkapa pamoja na mapungufu yake ya kibinadamu ila alikuwa thabiti kwenye fairness kwenye utawala wake na alichojali yeye ni utendaji tu. Mambo binafsi ya watu haikuwa kipaumbele kwake.
Sio huyu wa sasa ambae nasikia anafuatilia hadi watu wanachati nini na wanaongea nini.

Si huyu wa sasa ambae akisikia unaswali ofisini kwake ni nongwa na kosa.... refer to Prof Assad
 
Dau huyu huyu aliefuja miradi kibao ya nssf kama kule kigamboni walinunua viwanja kwa mamilioni ya fedha wakati thamani halisi haifiki 1M
Hizi ni fitina, huna ushahidi, unaongea usilo na ushahidi nalo na bado unalisimamia! Jambo usilolijua ni usiku wa giza. Kama dau alitenda hilo bila ya shaka Magufuli angemwadhibu.
 
Ni kipi kipimo cha kudeliver ambacho kinahalalisha kuvunja taratibu za kazi? Kila mfanyakazi akisema atumie resource za muajili kujenga sehemu ya ibada si itakuwa chaos.
Kwani inakuathili nini kuwa na sehemu ya kusali kwenye ofisi ya umma.
Kwa nini kwenye wimbo wa Taifa tunasema Mungu ibariki??? Kama tunakili uwepo wa Mungu kuna shida gani iwe wakristo au hata waislamu wakiweka sehemu yao ofisini kumuomba Mungu.

Mnajifanya mmestaarabika kumbe ni wabaguzi zaidi yaMakaburu
 
Dr Dau akiwa rais, Kipaumbele chake Cha kwanza itakuwa kuifanya Tanzania iwe nchi ya Kiislam. Jamaa ni mdini Sana. Haamini katika secular state.
Hili sio kweli, anaamini katika secular state, isipokuwa kimtizamo anaamini ipo namna ambayo watu wamebaguliwa kwenye nafasi na fursa kadhaa kwasababu tu ni waislam! Na ukimsoma between the lines utayaona hayo. Pia, sio dhambi kutetea imani yako pale unapoona inatendewe visivyo.
 
Ni

Ni kweli Kuna jamaa yangu yupo NSSF Morogoro aliwahi kunithibitishia hilo,Tena akaenda mbali zaidi akasema " Huku kwetu Nssf Kuna udini hataree,kupita hata idara ya utumishi chini ya Hawa Gassia" nakumbuka ilikuwa kipindi Cha awamu ya nne
tulifika pabaya...yule namba1 alitumika vby sn uku gasia (utumish wa nch nzma) wkuruganz kibao walijazn wnyew haohao. ubaguz k2 kbaya sn.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…