UPDATES: Mazishi ya marehemu Meshilieki Lendwala Mollel yamefanyika leo pale kijijini kwake cha Lesiraa Wilaya Arusha vijiji majira ya saa nane oo nusu mchana kwa kweli nimebahatika kuhudhuria na sikuweza hata kupata picha hata moja,na hakika nimepata kuwaona makaburu wa pale Snake Park ambao ndio marehemu alikuwa nao mpk mauti inamkuta na tetesi nilizopata ni kwamba hao matajiri wa Snake park wamehakikisha wanaisaidia familia ya marehemu A to Z na bila shaka imeleta faraja kwa familia iliyoachwa na marehemu wakati wanamhitaji. Lakini kilichofurahisha zaidi ni Ndg,jamaa na marafiki walivyojitokeza kwa hali na mali na kuacha shughuli zao tangu juzi na mpk leo bila ya kuchoka hilo imenitouch sana,Sina mengi sana ila baada ya yote nilimsikia Mtumishi wa MUNGU akisema Bwana ametoa na Bwana ametwaa!