Breaking News: Msanii wa taarab nchini Tanzania wa kundi la TOT plus, Mariam Khamis maarufu kama paka mapepe amefariki dunia usiku wa jana kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam mara tu baada ya kujifungua .Kuna habari za kusikitisha kwamba MARIAM KHAMIS amefariki dunia wakati wa kujifungua katika hospitali ya Muhimbili na mtoto amebaki mzima. Marehemu alikuwa star wa muziki wa taarabu kama "paka mapepe", "sitishiki na lawama zenu" na zingine kibao. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, Ameeen.