huyo jamaa alishawahi kunipigia namba hiyo ya tigo alijitambulisha kwa jina la honesty mgona Na ni afisa utumishi ofisi ya rais, aliniambia taarifa zangu za kutaka kuhama zimefika ofisini kwake, aliniuliza kama Nina undugu Na prof mwakyosi nilimjibu simfahamu ni ubin tu unafanana sina undugu naye Na wala simfahamu. akaniambia atanisaidia kwa vile anafahamiana vizur Na prof huyo hata kama sina undugu naye. mashaka yalianza pale aliponiambia nimtumie check namba, TSD namba Na file namba.
nilimuuliza kama taarifa zangu zimekufikia ina maana barua zangu za uhamisho mbona zina taarifa zote unazozitaka? alinijibu barua yako iliyofika INA namba ya simu tu ndiyo maana nimekupigia ili nipate details zaidi. nikamuuliza tena taarifa zangu umezipatje? akanijibu afisa utumishi wangu ndiye amezituma Na inawezekana ameziandika upya, nikamjibu barua niandike mm Nazi sign alafu mwingine aziandike upya? mbona mfumo huo wa utumish Tanzania hatuna umeanza lini? nikambia huyo afisa utumishi aliyekupa taarifa zangu Na aliyeandika barua yangu upya mpigie akupe details zangu zote nilizoandika kwenye batua yangu ya a wali. jamaa akamaind nataka nikusaidie unalet a ubishi akakata simu. hiyo namba yake tigo ninayo na line yake imesajiliw kwa jina nililolitaja hapo juu.
NB walimu wenzangu utapele huo upo nimeshuhudia watu wa4 wameibiwa, mmoja aliibiwa laki5, wawili laki Tatu tatu mwingine laki1, yaani huyu was laki5 alipata hadi barua ya tamisemi kumbe feki akapeleka kwa mkurigenzi ikasiniwa akafunga datasheet , akauza kila kitu akahamia mbeya. alipofika mbeya ndyo anaambiwa umeibiwa uhamisho wako feki rudi mbinga jamaa alichanganyikiwa. alirudi mbinga anapiga mzigo