Taratibu za kisheria za kufuata unapotaka kununua chombo cha moto ni zipi?

UMUNYU

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2017
Posts
726
Reaction score
564
Wanajf Ninaomba mnijuze taratibu za kisheria za kufuata ili kununua na kumiliki chombo cha moto mfano bodaboda.

Ninauliza kwa sababu wauzaji wamekuwa wengi,vinavyouzwa navyo ni mchanganyiko halali na visivyo halali!

Ubora nao ni nadra kuujua kwani "orijino na feki" navyo vinapatikana kundi moja!!Msaada tafadhali!!
 
Kutoka kwa mmiliki ni

1. Anayeuza sharti awe ndio anayesoma kwenye kadi
2. Uhamisho wa umiliki anayeomba ni mmiliki kwa kuandika barua kwa meneja TRA Mkoa husika
3. Itawapasa muwe na mkataba wa mauziano pamoja na risiti ya huduma ya wakili ili mkamilishe huo uhamisho wa umiliki.
4. Itakupasa uwe na TIN

NB: Kamwe usinunue piki piki kutoka kwa mtu ambaye hasomeki jina lake kwenye kadi halisi, pia usinunue piki piki inayoanza namba ya usajili na T mfano T 000 ABC huo usajili ulishafutwa kwenye piki piki na piki piki zinatumia MC mfano MC 000 ABC.

Kwa wauzaji na wasambazaji ni rahisi zaidi na haina mlolongo wa tahadhari sana.
 
Asante sana kwa ufafanuzi mzuri!Nitaufanyia kazi!Vipi kama nitaenda kwenye duka,vitu gani nizingatie?
 
Zingatia tu kuwa unauziwa chombo kipya na wewe ndio mmiliki wa kwanza. Uliza pia kama wanautaratibu wa kukusajilia, hapo watakuambia uwape TIN ili waitoe kadi kama wanautaratibu wa kukusajilia.

Kwa ujumla awe dealer aliyesajiliwa
 
Hapo kwenye kuhakiki ninafanyaje pia kujua kama haidaiwi!!Msaada tafadhali!Kwenye eneo hili mimi ni mgeni
Nenda kwa trafki Mwenye mashine cau ki tendo cha usalama barabarani,ataingiza Namba za gari utajua kama ina deni au lah,
 
Back
Top Bottom