Sasa naona Tanzanians ndiyo mnaanza kushituka, lakini its too late! suala la uhamiaji haramu si suala la Tanzania peke yake, hata unavyosema Kenya hakuna wahamiaji haramu sijui unatumia data za wapi, Binafsi nimefanya kazi mbalimbali kwa muda wa miaka mitatu, Uganda nimefanya kazi Miaka miwili, Rwanda, Zambia, Botwana, Nigeria, S.A, UAE, bila kutaja bara la ulaya na amerikana, achilia mbali Marekani amabako kulikuwa kimbilio kubwa kwa watanzani awengi hata siku za karibuni. Kinachotuua watanzania ni kuchagua kazi, na kufanya kazi kwa kutesti zali, watanzania wengi tuna tamaa, siyo rilayabo. Opotunities zipo kibao hapa tanzania, na suala la sisi kuzitafuta halipo, tumebaki kusema kila nafasi inayotangazwa itakuwa na mwenyewe! enzi za kuletewa barua ya ajira nyumbani kwenu zilishapitwa. Kuwalaumu Wakenya na wamalawi ni mwanzo wa chuki tu kama za wenzetu wa kule S.A, chuki zilizopelekea waafrika kuuana. Kama wewe bado umelala ujue ndiyo umeliwa, EAC inakuja kasi, kama haujaenda shule na haunakile ambacho soko la ajira linakitaka utabakia kuwa mwanasiasa wa kijiweni. Maisha ya sasa ni kupigana, Wakongo wanaona watanzania wanadharau sekta ya kosmetology kwa nini wasije kuchukua pesa? Sitetei wahamiaji haramu, ila tujue mhamiaji huangalie sehemu yenye fulsa nyingi za wazi. Cha kufanya ni kuhakikisha tu kkuwa Wageni wanaingia na kukaa kihalali bila kuvuruga amani, na hiyo ni kazi ya Uhamiaji.
Kama bado umelala amka mapema sana, mapema kabla serikali haijagundua kama inaupungufu wa nguvukazi na kuamua kutangazi watu wote wa dunia wenye ujuzi flani WAJE bongo (angalia mwakani UDOM itakuwa na Maprof. wangapi toka India), angali Rwanda ina waalimu wangapi kutoka Tanzania, angalia marekani ina machinga wangapi kutoka India. Tujifunze kusoma ala ma za nyakati na kubadilika kiujuzi na mori ili kukidhi mahitaji ya ajira na fulsa za kujiajiri. Bado mashamba yako mengi Ruvuma, Kigoma, Mara, Mbeya Iringa, na Morogoro, lakin i hatutaki kulima mpaka tupewe matrekta, ninani akupe trekta wakati hata hujakata miti, kama haujaandaa mradi kuwakonvisi wenye pesa kuwa biashara yako italipa!
Mi nadhani ingekuwa bora kabisa kama mahouse girl na wafagia barabara wote wangetoka malawi na Congo, halafu Malawi kukajaa Madaktari kutoka TANZANIA. Tuachane na chuki zisizomaana, unamchukia mtu kisa anafanya kazi ambayo wewe ullikuwa ukiitaka lakini hukuihangaikia. Sitaki kuamini kama shida na tabu za watanzai zinaletwa na Wamalawi au Wakenya, shida zetu zinaletwa na sisi wenyewe.