Taratibu za kufuata ili kupata TIN Number

Chuck j

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2011
Posts
2,366
Reaction score
828
Naombeni kwa mwenye kujua jinsi ya kupata TIN Number.
Asanteni


====================================


 
Nenda TRA,TIN hutolewa bure,ingawaje watakusumbua ili wapate kitu kidogo lakin komaa,usikubali kutoa rushwa,narudia tena usikubari kutoa rushwa,mtoa rushwa na mpokea rushwa wote ni watuhumiwa.TIN ni bure hata ukifika TRA utakuta matangazo ya kumwaga kukujulisha kuwa TIN hutolewa bure.Nakutakia mchakato mwema
 
TIN ni bure ila maagent wengi hukukamua hasa kama ukiwaachia wao wafanye. Kama unataka kutoa gari unaenda na kopi ya B/L pale TRA kodi za ndani pale jirani na TTCL posta. Utajaza application form na kusajiliwa katika computer then utapigwa picha na itaingizwa katika computer pia. Baada ya dakika kadhaa utapewa TIN yako. Jaza kitabu na potea hapo ni bure. Wakikuona kama haujui utaratibu watakuingiza katika mtego wa rushwa. Otherwise kama unataka TIN kwa ajili ya kubadili leseni then utaelekezwa uende TRA ya wilaya unayotoka ie Kino, Temeke au Ilala. Good luck
 
Duh ,,,,mi nataka kwa ajili ya kubadili renew lesen ya biashara ya mazao ya misitu,,umenisaidia sana,,Kama kuna kiachohitajika zaidi let me know pls,,Mungu akubarriki''
 
Kwa anayejua utaratibu anifahamishe na gharama zake pia...

Natanguliza shukrani
 
Kwa anayejua utaratibu anifahamishe na gharama zake pia...

Natanguliza shukrani

TIN number hutolewa bure lakini hupewi mpaka wakukadirie kodi kulingana na biashara yako ilivyo then baada ya kulipa kodi ya awamu ya kwanza ndio wanakupa TIN number kuhusu leseni nenda manispaa ya kinondoni for more details au wadau watajazia.
 
TIN number hutolewa bure lakini hupewi mpaka wakukadirie kodi kulingana na biashara yako ilivyo then baada ya kulipa kodi ya awamu ya kwanza ndio wanakupa TIN number kuhusu leseni nenda manispaa ya kinondoni for more details au wadau watajazia.

nashukuru mkuu...
 
umeshajisajiri jina la biashara yako,? kama bado nenda brela kajisajiri na TIN no wanatoa bure ila mpaka wafanye installment ya biashara yako ndiopo wakupe, hiyo na kuhusu leseni ya biashara mpaka uwe na TIN no ndipo waweza jaza fomu za leseni ndipo waje kukagua eneo au biashara yako iilipo wakupe leseni? una jingine la kusema?
 

Hapo kwenye blue sijaelewa vizuri.
TRA mpaka wafanye nini ndio wakupe TIN ?
Ina maana TIN inatolewa kwa masharti fulani ?

Naomba msaada wa kueleweshwa.
 
kwani aliyeuliza ni tindikalikali au ni mu-israel mtoa roho za watu?
Hapo kwenye blue sijaelewa vizuri.
TRA mpaka wafanye nini ndio wakupe TIN ?
Ina maana TIN inatolewa kwa masharti fulani ?

Naomba msaada wa kueleweshwa.
 
kwani aliyeuliza ni tindikalikali au ni mu-israel mtoa roho za watu?

Nimeona mada nikaona kuna jambo sijaelewa vizuri nami labda naweza kuelimishwa.
Ndio maana nikauliza tu hapo.
Nitafurahi kama nitaelimishwa zaidi kwenye mada hii ingawa sio mimi nilioanzisha mada hii.
 
oky kama umejisajiri jina la kampuni/biashara yako unayotaka kufanya, nenda TRA watakupa fomu za TIN utajaza na watakupa maelekezo yote waoo namna ya kufanya utapataa maelekezo na mambo mengine palepale ni hayo mkuu
Nimeona mada nikaona kuna jambo sijaelewa vizuri nami labda naweza kuelimishwa.
Ndio maana nikauliza tu hapo.
Nitafurahi kama nitaelimishwa zaidi kwenye mada hii ingawa sio mimi nilioanzisha mada hii.
 
Ingia tovuti ya tra, nenda ujazaji online wa tin, fuata maelekezo, ukimaliza nenda tra kuweka dole gumba. Maelezo mengine ya upatikanaji wa tin utapata tra bila wasiwasi kabisa. Ukipata tin nenda halmashauri yako kitengo cha biashara watakuelekeza ujazaji wa fomu na mengineyo, ila si bure tena ni fedha, gharama yake itategemea kule tra walikufanyia makadirio kiasi gani ya biashara yako kwa mwaka. ( wakati mwingine tra wanakwambia uende kwa tax consultant akufanyie makadirio ya mapato yako kwa mwaka, then consultant ataandika report utakayopeleka tra ili ufungue file na ulipie tax in advance).
 
Nawashukuru sana wachangiaji wote katika mada hii...hakika itanisaidia sana.
 
Mimi natafuta mtu anaye weza kunisaidia kupata TIN Number na Lesen ya biashara-
 
Mbona unapenda short cut ndugu?nenda tra ukapate tin then nenda manispaa kapate leseni.very simple.
 
Kwa mdau aliye mbali inakuwaje??
 
Tafadhali check me asap kama unaweza kunitolea TIN number maana kwa sasa sipo karibu na mji na inahitajika sana a muhimu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…