Wakuu wa JF,
Msaada wenu unahitajika:
1. Naomba kujua taratibu za kupima kiwanja dar es salaam ikoje? Process inakuwaje na cost?
2. Kupata leseni ya makazi process yake ikoje?
Asanteni
Ungeweka udaku hapa au habari zinazohusu kufunguana zipu, weeee, ungeona thread inajaa by the second.
Mie nilichoka nilipoambiwa bei ya kupimiwa chapchap (rushwa) ni 2.5 million.
Otherwise kuna kama miezi sita ya kusubiri kikao cha madiwani na ujinga mwingine kama huo ambao hata sikuwa na moyo wa kuusikiliza vizuri samahani.Nikakataa kutoa rushwa. Nikaelewa matatizo ya serious investors.
Kama kabwela mie naombwa (more like napewa "bei" ya rushwa inayotakiwa) 2.5 milioni, investor anayetaka kuanzisha a genuine multi million dollar business?
I suspect walikuwa wananitisha tu kutaka kunitoa hela, wakanikuta mtu mwenyewe sina shida hivyo sikufuatilia sana, to the chagrin of input seekers on this thread.
I am watching this space. I am also wondering if the NHC apartments are worth it, especially considering the commutes.
Ungeweka udaku hapa au habari zinazohusu kufunguana zipu, weeee, ungeona thread inajaa by the second.
JF ndivyo walivyo, angalia thread za ngono, zitachangiwa mpaka.........pages 40 and above. Weka thread ya sheria, afya, lo watu wawili/watatu, kama hii hakuna mtu. MMU utachoka utitili wa michango! The oldest trade made by human being was related to sex! ANYWAY KUPANGA NI KUCHAGUA
Sasa mbona unatoka nje ya mada? Toa darasa bana acha longolongo mingi kama Pinda.
1 KITENGO CHA MIPANGO MIJI AFISA MIPANGO MIJI(TOWN PLANNER) Kuandaa michoro ya ubunifu ya mipango miji ya maeneo ambayo itaratibu uendelezaji wa mji husika.(inaitwa town planning drawings inshort TP) Kubadilisha matumizi ya ardhi ya viwanja ambavyo vimeshapewa hati Kutoa vibali vya ujenzi wa majengo Kutoa vibali vya upimaji wa ardhi Kufanya marekebisho ya michoro ya mipango miji Mchoro wa mipango miji ambao unaonyesha matumizi mbali mbali ya eneo husika e.g shule, open spaces etc ukishatayarishwa na manispaa ni lazima upelekwe wizarani kwa mkurugenzi wa mipango miji wa wizara ya ardhi ili audhinishe. 2 KITENGO CHA UPIMAJI AFISA UPIMAJI (LAND SURVEYOY) Kazi kubwa ya mpimaji ni kupima eneo ambalo tayari lina mchoro wa mipango miji na anatakiwa kupima kulingana na mchoro wa mipango miji kama unavyo eleza. Upimaji uatendana na mambo yafuatayo Atapanda mawe(beacons) Atakupa kiwanja namba(plot number) Ataonyesha ukubwa wa eneo plot area) Ataonyesha na mipaka ya kiwanja(plot boundaries) Ramani ya upimaji inayo onyesha mawe ya kiwanja, kiwanja namba, ukubwa wa kiwanja na mipaka ya kiwanja ambayo lazima iwe imesajiliwa na kuidhinishwna mkurugenzi wa upimaji na ramani wa wizara ya ardhi 3 KITENGO CHA ARDHI AFISA ARDHI(LAND OFFICER) Majukumu ya huyu bwana ni Kuandaa hati miliki ya viwanja ambavyo vimeshapimwa na ili aanze kukuandalia hati utatakiwa umpelekee mchoro wa mipango miji unaonyesha kiwanja chako ili ajue matumizi yake, ramani ya upimaji ya kiwanja chako ili ajue anaanda hati ya kiwanja gani, kipo wapi na kina ukubwa gani coz wanapokadiria kodi ya kiwanja lazima wajue ukubwa wa kiwanja. Kazi nyingine ya afisa ardhi ni kuhuisha miliki yani kuongeza mda wa umilikiwa ardhi mana kuna hati za miaka 33, 66 na 99. Kazi nyingine ni kuhamisha miliki kutoka kwa mmiliki mmoja na kwenda kwa mwingine inaitwa transfer. Hati nayo ikisha kamilika kuandaliwa na manispaa ni lazima ikahakikiwe na kamishna wa ardhi wa wizara na hatimaye msajili wa hati naye ataisajili. NB: mara nyingi gharama za kupima kiwanja kimoja ni kati ya laki 800000 hadi 1000000/- lakini bei huwa inapungua mkiwa zaidi ya mtu mmoja mana mtakuwa mnashare gharama. Kwenye suala la upimaji wa viwanja hakunaga vikao vya mipango miji ila kazi zote za mipango miji ni lazima ziinishwe na kamati ya mipango miji ya manispaa kabla ya kuwasilishwa wizarani. Kwa mawasiliano zaidi na uelewtuwasiliane through 0779000250. Nawasilisha

Tunashukuru kwa ufafanuzi wako mzuri ngoja nijipange ili niwaone hao TP.gharama ya kuandaa hati kwa malipo halali ya serikali haiwezi kuzidi laki 300000/= kwasababu utahitajika kulipia fomu ya kuomba kumilikishwa ardhi kutoka ofisi ya ardhi ya wilaya au manispaa ambayo ni elfu 5000/=, utahitaji kulipia kodi ya ardhi(land rent) kwa mwaka ambayo itategemea thamani ya ardhi ya eneo husika na ukubwa wa kiwanja ambayo mara nyingi haizidi laki mbili na mwisho gharama ya kuandaliwa deed plan(raman ya hati) ambayo nayo haizidi elfu50.
ushuari wangu bei sijui ila nenda wizarani pale ongea na mshkaji unayemfahamu kwani process inaweza kukugharimu ama isikugharimu lkn taratibu za awali ni hizi hapa
nenda serikali ya mtaa wakuandikie kitu inaitwa muhutasari wa kuomba kupimiwa eneo. hii huwaga wana chaji 10%ya bei ulonunulia eneo na wanakupa risiti but kwa uzoef wangu naona hata vitabu vyenyewe vya risiti havikaguliwi so ni kama za kwao tu. ukiongea nao vzr wanaweza kupunguza bei.
baada ya hapo kagua eneo lako kama kuna jirani ambaye amepima eneo lake so ana beacon kama yupo soma namba za jiwe zinaandikwaga juu kabisa mf ZN 49 etc.
kama hakuna basi hapo tafuta mtu wa jikon kabisa kule ardhi mweleze nia yako achukue GPS aje apime coordinates kwenye engo zote za eneo wao watakwenda kuingiza kwenye master pln waone kama lina mchoro kama halina jua unatakiwa kugharamia mchoro ila kama upo basi kazi kwako ni rahisi sana.
wakishajua kama halijapimwa ndipo watakapo kuambia nini cha kufanya so b4 kwenda savei kwanza eneo lako ama kuna beakon ili ujue itakugharim nini hasa.
usitishwe na bei bana kila ktiu kinazungumzka ila usiende ka hawa private consultants watakulima miele kibao nenda huko front usogope. pia kama eneo haliihitaj ramani basi muda ni mchache sana unakuwa umepata hati na mawe. manake watakupa ofa kisha ndipo kama baada ya miez 2 unapata title deed. ni vitu ambavyo vinafanyika bana ila wanaotaka kupitia kwa hawa wa private wanapigwa na unakuta hata baada ya miaka 2 bado title deed hajapata.