Taratibu za kusimamisha leseni ya biashara kisheria kwa upande wa TRA na Manispaa

Taratibu za kusimamisha leseni ya biashara kisheria kwa upande wa TRA na Manispaa

pangakali 2

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2019
Posts
239
Reaction score
221
Kutokana na kushuka kwa biashara yangu imeniwea ugum hadi katika uendeshaji wake kiasi cha kuanza kukopa huku na kule na kuongeza mzigo lakini jitihada zimegonga mwamba.

Msaada mwenye kujua taratibu za kusimamisha leseni ya biashara kisheria kwa upande wa TRA na Manispaa. Nisubirie upepo huu upite na kujipanga upya.

Fika ofisi za TRA ulipo sajili biashara yako utapata muongozo na vitu vya kufanya, ila kwa ushauri tu kama biashara haieleweki lkn unaona mbele inaweza kueleweka ni heri uwe unapeleka taarifa za kutokufanya biashara/mauzo kuliko kuisimamisha/kuifunga kwa muda,

Process za kuanza kuirudisha tena zitakugharimu zaidi, tafuta auditors wakuandikie hamna ulichoingiza kwa kipindi hicho uwasilishe TRA.

kila la kheri chief.
 
Kwa tra nenda ofisini kwao(pale ulipolipia kodi) watakupa maelekezo kuwa uandike barua ya kusitisha biashara yako kuilekeza kwa kamishna. Kwa manispaa sijajua utaratibu wao.
 
Leseni ina-expire kila mwaka kwahio itakwisha yenyewe hauta-renew..., Mapato TRA andika Barua kwa Kamishna wa TRA kwamba unasitisha kwa muda na sababu peleka ofisini kwao.., Usisahau kubaki na copy yako hao jamaa hawachelewi kusema file limepotea na barua imepotea.., Siku ukija kuendelea utakuwa na kithibitisho cha copy ya barua uliyowaandikia
 
Habari zenu Jamani, kwa anaejua anisaidie kunifahamisha hatua za kufuata ili kurudisha leseni ya biashara.
 
Back
Top Bottom