Suala hilo limeegemea katika Sheria ya Ajira na Uhusiano kazini(Employment and Labour Relations Act No.06 of 2004) na pia sheria ya Labour Institutions Act No.07 of 2004 vilevile na sheria ya Employment and Labour Relations( Code of Good practice )Rules GN. No.42 of 2007.Hivyo kwa kuzingatia tatizo hilo kwa mujibu wa sheria hiyo ya kwanza No.06,sababu ambazo zinaweza kufanya muajiriwa afukuzwe kazini ni kufanys kosa ambalo ni kinyume na makubaliano ya kimkataba(misconduct),kosa hilo linaweza kuwa wizi,ama kufanya kazi kinyume na maagizo au kufanya kazi chini ya kiwango(work below the skills/standard), ama kufanya kosa lolote ambalo sheria hizo hapo juu zinamruhusu kumfukuza kazi(lakini kwa kuzingatia utaratibu wa kumfukuza kazi).Vilevile jambo la muhim hapa ni kuwa hatakama muajiriwa amefanya makosa hayo kiasi ambacho sheria insmruhusu kumtengua ajira bado muajiriwa atalazimika kuthibitisha makosa hayo kwa kumpa notisi ya kumuita na ampe haki ya kumsikiliza utetezi wake.Vile vile muajiri anaweza kumfukuza kazi au kumtengua kweny ajira bila hata ya kufanya kosa lakini katika mazingira kama; rudundancy operation(hali ya kupunguza wafanyakazi kenye eneo la kazi kwa kuzingatia cheo na idadi), au endapo mfanyakazi ameugua kwa mda mrefu sana kiasi ambacho kutokuwepo kwake kazini kunapelekea kuyumba kwa ufanisi na mchakato mzima wa uzalishaji mali,ingawaje haya yote laxima muajiri afuate taratibu maalum kwamfano suala la kutaka kupinguza wafanya kazi(redundany) ni lazima afanye haya:
1) kumpa notisi muajiriwa huyo ya kumjulisha kuhusu kuondolewa kazini
2) kumpa sababu za msingi kwanini anamuondoa kazini
3)kumpa nafasi ya kujiandaa kutafuta ajira nyingine kwa kumpa mda maalum na wakutosha.
4) na kuzingatia mkataba unasema nini juu ya matokeo ya kufanya redundancy.
Hivyo ikumbukwe kuwa muajiri akishindwa kufuata utaratibu wa kumuondoa kazini muajiriwa mahakama au bodi yoyote inayohusika na kusuluhisha migogoro ya wafanyakazi inaweza kumuamuru musjiri haya:
1)kumrudisha kaxini muajiriwa na kumlipa fidia ya pesa ya mshahara wa miezi 12,au kumlipa malipo yote aliostahiki kulipwa kwa kuhesabu tangu siku anafukuzwa mpaka amri inatolewa na mahakama/bodi.
2)kumlipa tu fidia ya mshahara wa miezi 12.
Kumlipa fidia ya mshahara wa miezi 12 na kubadilisha vipengele vya mkataba.