Habari Wana JF.
Nina shamba langu wilayani Biharamulo mkoa wa Kagera lenye ukubwa wa ekari 34 na lina miti mingi ya asili kama vile mibanga, minazi, misindo n.k.
Nahitaji kuivuna na kuichoma mkaa na kwa makadirio zitapatikana takribani junia(gunia) 400.
Sasa naomba mwenyekujua gharama zote za leseni, vibari na usafirishaji anijuze hapa.
Nimepitia website ya tfs lakini sikuona walipo bainisha gharama zao.
Nahitaji kuuleta hapa Dar es salaam.
Naomba elezea as if sijui chochote.
Habari! Nimefanikiwa kuanza biashara hii recent, hizi ndo hatua nilizopitia:
1. Kwanza kabisa unatakiwa kupata kibali cha uvunaji wa mazao ya misitu kutoka Halmashaur husika shamba lako lilipo, na hicho kibali kinaanza kwa wewe kupata ruhusa kutoka serikali ya kijiji/kata, ambapo watakaa na kutengeneza muhtasari unaonesha kwamba wao kama kijiji wamepitia na kuridhia wewe kuvuna miti shambani kwako kwa sababu ambazo wewe utataja, ndani ya muhtasari huo watatja na makadirio ya miti utakayovuna.
2. Utajaza form ya maombi wilayani ambayo utailipia 170,000 kama sikosei, kwa sasa vibali vinatoka mara moja tu kwa mwaka, mwanzo wa mwaka wa fedha wa serikali, I mean kuanzia July, na machakato ni kwamba, baada ya wewe kujaza form, halmashauri wanakaaga kikao kupitisha vibali mwezi wa sita, utajulishwa kama maombi yako yamepita au lah! Kma yamepita utapewa control number kulipia kibali, kwa wilaya niliyopo mimi nimelipia 265,000/TZS
3. Utaenda kuvuna miti yako na kuchoma mkaa
4. Ukishachoma mkaa, unarudi wilayani ku declare idadi ya gunia ulizopata kwa ajili ya malipo ya bidhaa kwa gunia, wilaya niliyopo mimi wanatoza 20,000 kwa kila gunia kubwa ulilopata. Bila kibali hiki huwezi kupata kibali cha kusafirisha.
5. Utajaza na kuomba leseni ya kufanya bishara katika wilaya unayokwenda kuuza mkaa kupitia mfumo wa TAMISEMI, unaoitwa TAUSI, Leseni ya kuuza Mkaa Jumla na Rejareja kwa sasa ni 300,00/ Kwa mwaka.
6. Utaomba kibali cha kusafirisha Mkaa ambacho kinakatwa kwa gari, inategemea na ukubwa wa gari (Hichi mara nyingi wenye magari ya kubebea mkaa wanacho, hivyo ukibahatika kumpata mwenye kibali, unatembea na upepo chap! Lakini pia sio gharama sana kupata kibali hiki, kwa Fuso ni kama 21,500/ tu)
Hapo utakuwa upo huru kuuza mkaa bila buguza yeyote!
N:B
Nimeuza Mkaa Mabibo sokoni kwa sh 77,000/ kwa gunia kubwa kwa bei ya jumla. Nimetengeneza faida ya kama 39,000 baada ya kutoa jumla ya gharama zangu zote ikiwemo wakata visiki (wasafisha shamba) ambao niliwalipa kwa heka 140,000, wachoma mkaa ambao walinichaji 4500/ kwa kila gunia walilolotoa, usafiri kutoka porini had Dar, gharama zangu za malazi na chakula nilipokuwa porini, gharama zangu za mafuta ya gari langu kila nilipokuwa naenda shamba n.k.
Inalipa zaidi kama ukiwa na store, manake ukiwa huna haraka, kwa sasa Dar gunia kubwa la mkaa linaenda hadi 100,000/ mimi sikuwa na stoo, so ilibidi tu nikubaliane na bei ya madalali.
Haikuwa plan yangu kuuza mkaa, plan ilikuwa kama wewe kuandaa shamba kwa ajili ya kilimo, ila kwa sababu nina vibali tayari, na nimeona kuna hela, rasmi nafungua stoo Dar.. Nitauza mkaa, nasema tena, nitauza mkaa