Tareha 26/04/1964 ni siku ya msiba mkubwa kwa Wazanzibar

dega

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2012
Posts
3,172
Reaction score
3,082
(1) Tarehe 26/04/1964 Ndio siku ambayo Jamhuri ya Watu wa ZANZIBAR iliuwawa [State death]

(2) Tarehe 26/04/1964 Ndio siku ambayo Wazanzibar walipoteza mamlaka yao [Sovereignty] ya Nchi yao.

(3) Tarehe 26/04/1964 Ndio siku Wazanzibar walipoteza uraia wao [CITIZENSHIP] wao.

(4) Tarehe 26/04/64 Ndio siku ambayo Rais wa JAMHURI YA WATU ZANZIBAR alikoma [cease]kuwa Amiri Jeshi Mkuu.

(5) Tarehe 26/04/1964 Ndio siku Wazanzibar walipoteza kitu chao UMOJA WA MATAIFA.

ANGALIA:

# ZANZIBAR imetoka kuwa DOLA hadi MKOA.

#Uzanzibar umetoka ktk hadhi ya URAIA hadi UKAAZI.

#Rais wa ZANZIBAR kutoka Amiri Jeshi Mkuu hadi KAMANDA MKUU WA IDARA MAALUM.

#Kutoka Rais wa DOLA YA ZANZIBAR hadi WAZIRI ASIYE NA WIZARA MAALUM.

#ZANZIBAR kutoka mwanachms wa U.N hadi kukataliwa kujiuna na FIFA.

JUWA KWAMBA:
#Hakua kitu chochote Duniani kitakachoweza kufidia Wazanzibar kupoteza Utaifa wao.

#Hakuna kitu chochote Duniani kitakachoweza kufidia Wazanzibar kupoteza Dola yao

#HAKUNA KITU CHOCHOTE DUNIAN KILOCHOWEZA/ KINACHOWEZA/KITAKACHOWEZA KUFIDIA HASARA WALIOIPATA WAZANZIBAR TAREHE 26/04/195
SIKU YA MSIB MZITO.
 
Sasa iweje? Muungano umeifukuzilia mbali mifumo ya kisultani. Mabaki ya usultani ndiyo yanayoshupalia muungano uvunjwe. Kama si muungano Zanzibar haiwezi kuwa moja, Unguja na Pemba watasumbuana tu. Pemba watataka kuwa na jamhuri yao. Inafaa sana visiwa hivi viendelee kuwa kwenye huu muungano kwa karne nyingi ili kuwaweka wazanzibar pamoja daima
 
Matatizo ya kufikirika ya wazanzibari yanakukera nini wewe mTanganyika ?! Shida ya nchi mawazo ya Nyerere ni kama msahafu
 
Tulieni wazanzibar,acheni kushtukashtuka,,
Mko salama ndani ya jamuhuri ya muungano wa tanzania,
fanyeni kazi tujenge na kuimarisha muungano wetu,,
 
Usitugawe we punguani wahedi.. Unajua kwamba wazanzibari wengi asili yao ni tabora, usukumani na unyanyembe, e.t.c

Sasa Ukitaka kututenga na ndugu zetu tutakunyofoa hizo kengele zako mbili hapo chini.
 
pasingekua na mapinduzi zanzibar bila watanganyika kuhusika..
 
Wazanzibar mna inferiority complex sana...

Mbona hayo yote watanganyika waliyapoteza na hawalii kama wewe.
 
Matatizo ya kufikirika ya wazanzibari yanakukera nini wewe mTanganyika ?! Shida ya nchi mawazo ya Nyerere ni kama msahafu
Ingekuwa rahisi wazanzibar waoneshwe mlango wa kutokea wajitawale wenyewe, sultani atarudi Zanzibar haitakuwa moja, haya mambo si ya kufikirika yako dhahiri. Masalia ya utawala wa kisultani yapo, ndiyo hao wasioutaka muungano. Wanafahamu hawawezi kupindua serikali muungano ukiwepo. Sultani hakupenda kupinduliwa naye anataka kupindua arudi kutawala. Sasa nani azembee avunje muungano? Vurugu zitakazotokea ni aibu kwa taifa. Muungano Udumishwe Kwa Usalama Wa Taifa
 
Sasa iweje? Muungano umeifukuzilia mbali mifumo ya kisultani. Mabaki ya usultani ndiyo yanayoshupalia muungano uvunjwe. Kama si muungano Zanzibar haiwezi kuwa moja, Unguja na Pemba watasumbuana tu. Pemba watataka kuwa na jamhuri yao. Inafaa sana visiwa hivi viendelee kuwa kwenye huu muungano kwa karne nyingi ili kuwaweka wazanzibar pamoja daima

Acha kuishi na kasumba mbovu mwana Lumumba
 
Usitugawe we punguani wahedi.. Unajua kwamba wazanzibari wengi asili yao ni tabora, usukumani na unyanyembe, e.t.c

Sasa Ukitaka kututenga na ndugu zetu tutakunyofoa hizo kengele zako mbili hapo chini.

Wengi wepi hao labda ungetusaidia mifano
 
Ingekuwa rahisi wazanzibar waoneshwe mlango wa kutokea wajitawale wenyewe, sultani atarudi Zanzibar haitakuwa moja, haya mambo si ya kufikirika yako dhahiri. Masalia ya utawala wa kisultani yapo, ndiyo hao wasioutaka muungano. Wanafahamu hawawezi kupindua serikali muungano ukiwepo. Sultani hakupenda kupinduliwa naye anataka kupindua arudi kutawala. Sasa nani azembee avunje muungano? Vurugu zitakazotokea ni aibu kwa taifa. Muungano Udumishwe Kwa Usalama Wa Taifa
Bado nakuuliza wewe mTanganyika, aina ya uongozi na kiongozi wanaemtaka awaongoze wao waZanzibari inawakera nini waTanganyika ?!. Kwanini hatukukerwa Malawi chini Rais wa maisha Dr H K Banda, au Kagame, Nkurunzinza, Museveni na Uganda yake au Nyang'au wa Kenya ?!. Kwanini lazima Zanzibar iongozwe kutokea Dodoma ?!
 
Back
Top Bottom