Tarehe 20/07/2020 sitaisahau, mbaya kwa watia nia nzuri kwangu

Tarehe 20/07/2020 sitaisahau, mbaya kwa watia nia nzuri kwangu

WENYELE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
1,433
Reaction score
1,442
Wakuu natumaini mko salama

Niende moja kwenye mada. Tarehe 20/07/2020 ilikuwa mbaya sana kwa watia nia hasa Kigamboni.

Nami upande wangu kabla jua halijazama ilikuwa mbaya sana.

Kwanza kabla ya hapo COVID-19 ilikuwa imeniathiri, nilikatwa mshahara ili kuwasaidia watu wa chini yangu nao wapate chochote sababu biashara yetu imeyumba so ilibidi uongozi ukate mishahara ya watu wanaopata zaidi ya milioni moja ili kuwalipa wafanya kazi wanaopata kipato chini ya laki tano.

Lakini Mungu sio Dkt. Mashinji, wiki iliyopita siku ya ijumaa nilifanya interview moja na shirika moja hivi la kimataifa, nilifanya vizuri na majibu wakasema watanipa 20/07/2020

Kazi yenyewe sio permanent ni ya mwezi mmoja tu; malipo niliwaambia wanipe $300 kwa siku, lakini ilipofika 20/07/2020 nilikuwa wamenitumia email kuwa malipo niliyosema ni makubwa sana na si halali kwa uzoefu wangu na pia kutokana na nchi ninayotoka, wao wakasema watanipa $200 kwa siku.

Nilipoona hivyo wakati huo Kigamboni mnyukano unaendelea, nilihofia kupoteza hii kazi, niliishiwa nguvu wakati huo nafuatilia mtanange wa Kigamboni, mimi ndo nikawa na presha kuliko hata mtoto wa baba.

Kwa kuona hivyo niliamua kukubali tu $200 kwa siku,nikawajibu nimekubali fasta, nimekaa kidogo nikatumiwa email nimechaguliwa. Sikuamini kwa kuwa ndo mara yangu ya kwanza kupata kazi ya malipo makubwa hivyo kwa muda mfupi.

Muda huo huo ikabadili mood yangu, nilitoka kijasho cha furaha na kwenda kuharusha (nimeamini furaha na huzuni zina hisia na response inayofanana) niliwajibu kuwashukru na siku ya jana nilikuwa nakamilisha kusaini Makabrasha yao na sasa hivi nasubiri wanifanyie training ili nisaini mkataba.

Kiukweli nilikua down sana, kipato kiliyumba ila Mungu kaniletea mshahara wa miezi kadhaa kwa mwezi mmoja tu huku nikiendelea na kazi yangu ya awali kama kawaida

Mungu ni mwema, yeye ndo anajua wapi anatupeleka, ukiwa na huzuni wewe wengine wanakuwa na furaha.

Mungu awabariki vijana wapambanaji wote ipo siku utasherekea matunda ya jasho lako.

NB: Kazi yangu ya awali naendelea nayo kama kawaida maana hii kazi niliyopata ni consultancy, so naifanya nikiwa kazini hata nimekaa na boss wala hata jua.
 
Au wewe umeajiriwa katika kamati ya ccm yakuwala watu vichwa kama mzee makonda na wengine.
 
Najua kuna watu watataka kujua kazi gani hiyo unalipwa pesa ndefu hivo kwa day [emoji2][emoji2][emoji2] jibu ni ....akili ku mkichwa
 
Najua kuna watu watataka kujua kazi gani hiyo unalipwa pesa ndefu hivo kwa day [emoji2][emoji2][emoji2] jibu ni ....akili ku mkichwa
Mkuu mimi ni consultant sema awali nilikua nafanya kazi kwa hela kiduchu...hata wewe km una kazj unaweza nipatia tu
 
Laki tano kwa siku mara mwezi mmoja inakuja milioni 15. Sio haba.

Kule kwetu Iringa unapata kiwanja Kigonzile na kujenga nyumba hadi inaisha.
 
$200 per day

unawashauri kutengeneza Atomic.!!

ww jamaa ni ndugu yangu kabisa,tutafutane broh
 
Back
Top Bottom