Kura yangu ni moja tu, lakini moja ya kwangu na ya mwingine, na mwingine, zitakuwa kura mamilioni.
Sikufikiria kupiga kura. Sikujishughulisha na kuhamisha taarifa zangu. Lakininsasa sina namna. Nimeamua kuondoka tarehe 26 toka Dar kwenda kanda ya Ziwa ili kura yangu ya kumpa Lisu isipotee. Nitasafiri umbali wa zaidi ya 1,400km kwenda kumpigia Lisu kura. Ole wake mtu aibe kura hii ya gharama kubwa. Nitabakia huko huko mpaka niyapate matokeo.