1. Sio kila Gen-z walioandamana walifanikiwa kuiondoa serikali madalakan au jeshi liliwaunga mkono.
Tunaangalia tu Madagascar, Nepal au Bangladesh, lakini kuna nchi kadhaa ambazo wananchi walishindwa kuiondoa serikali. Na haijachukua siku moja, inafika hadi miezi n. K
2. Kuna nchi kama Kenya, Indonesia, wananchi waliandamana lakini hawakufanikiwa kuiondoa serikali.
3. Kuna nchi kama Myanmar ambayo mpaka sasa imegeuka kua vita kabisa ya risasi.
Watanzania wana imani kubwa sana na JWTZ kuliko uhalisia wa jeshi hilo, pia wanachukulia suala la kuiondoa serikali dhalimu ya Samia kama jambo jepesi.
Pia ni muhimu kujua kua vyeo vya juu vya jeshi, ni vya kisiasa zaidi, hawana tofauti na Samia mwenyewe.
Huenda bado wananchi hawako tayari au hawafahaku magnitude ya kile wanachotaka kukiendea
Kuamini kwamba tarehe hiyo kuna mtu ataandamana ni kujifanya kipofu wakati unaona. Maandamano ili yawe effective yanahitaji kuwa na viongozi waratibu na kundi kubwa la watu walioko pamoja na wenye malengo sawa na wenye kutii na kusikiliza sauti na mamlaka ya huyo kiongozi
Kwa hiyo hapa ni rahisi kujua kwanini hakuna maandamano
Kuhusu wananchi kulitegemea jeshi au jeshi kuwategemea wananchi, haya ni matumaini hewa. Jeshi labda liamue lenyewe huko huko lakini sio eti kwasababu ya hiki kinachoendelea
Hakuna jeshi lenye nia ya kuondoa serikali madarakani tusidanganyane. Kama hiyo nia inakuwepo kwetu raia itakuwa kama surprise.
Kuhusu Gen Zi, labda tusubiri kizazi cha tatu kutoka sasa lakini sio hiki kizazi cha kubeti na UTI
Ila nachoamini kwa hakika kitatokea ni moja au machache kati ya haya:-
1. Wao kwa wao huko ndani ya jumba kuu kuvurugana na pengine kupelekea baadhi ya kulazimishwa watu waamini wamependwa zaidi kwenda ambako kila mmoja ataenda
2. Mtawala kutawala kwa hasira na visasi kwasababu anajua kundi kubwa halimpendi na haliko upande wake
3. Matukio kama haya ya kina Polepole yataongezeka zaidi
4. Chadema kukumbana na misukosuko mikubwa zaidi ya hii ambayo inaendelea sasa jambo litakalo wakatisha tamaa wengi
5. Wale waliokimbia kipindi kile wapo watakao fanya hivyo tena
Mambo yanaweza kwenda vuruluvarala kwasababu ya Panic za mamlaka