Tarehe 31 Machi, 2022 TTCL wanapandisha bei ya vifurushi

Tarehe 31 Machi, 2022 TTCL wanapandisha bei ya vifurushi

Status
Not open for further replies.

Ferruccio Lamborghini

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2020
Posts
1,667
Reaction score
2,595
Noma sana wakuu, tarehe tajwa hapo juu 31.03.2022, shirika la serikali la mawasiliano litatupiga na kitu kizito sana kichwani, wanapandisha vifurushi.

Bufee inaweza kuondolewa maana inawatia hasara tu. Toboa night HAIRUDISHWI ng'o

Si mnakumbuka tuliambiwa tuhamie Burundi tukaanza kuleta mapozi?🤣

Sasa nyumbani kunafuka moshi.

Tujiandae kisaikolojia.
 
Mimi natupa laini yao watu wenyewe hawana network ila vifurushi ni mserereko.
 
Cherokee
 
Attachments

  • IMG-20220329-WA0014.jpg
    IMG-20220329-WA0014.jpg
    34.7 KB · Views: 21
Watanzania tunalalamika saaaaaana. Ila kiukweli ni moja ya nchi chache DUNIANI ambazo unapata bando la uhakika chini ya USD 1. Ni nchi chache sana zina kiwango hiko. Tuwe na shukrani.
 
Watanzania tunalalamika saaaaaana. Ila kiukweli ni moja ya nchi chache DUNIANI ambazo unapata bando la uhakika chini ya USD 1. Ni nchi chache sana zina kiwango hiko. Tuwe na shukrani.
Na tunaishi chini ya Dola 1.
usisahau hilo.

ulaya huko bei ya mafuta na gesi imepanda wamelalamika. Huku kwetu ni nani tusilalamike walau kwenye bando tu?
 
Niliweka salio siku nimeisajili sijarudia tena maana sikupenda huduma yake. Labda kwa sababu laini moja ya Zantel ilikata kiu ya mawasiliano.

Ila naona kuwa kuna aina fulani ya haya makampuni ya mawasiliano kupokezana vijiti katika upangaji wa bei za vifurushi. Huyu akibana anaachia mwingine ili kuongeza idadi ya subscribers.

Zantel wametesa weeeeeeeh kama mwaka mzima nikaona duh huu ndio mtandao nikasahau shida za vodacom, baadae wakabana. Nikahamia tigo kwa sasa saizi yako angalau unajikadiria.

Hata hivyo, tutegemee bei kuongezeka zaidi kwa sababu ya vita kati ya Urusi na Ukraine. [emoji12]
 
Watanzania tunalalamika saaaaaana. Ila kiukweli ni moja ya nchi chache DUNIANI ambazo unapata bando la uhakika chini ya USD 1. Ni nchi chache sana zina kiwango hiko. Tuwe na shukrani.
Unaongelea 1 dollar kununua bando, wakati ni pato ambalo kwa mwananchi wa kawaida ni kipato cha wiki. Uchumi wetu kwa wengi upo chini sana.
 
Mtandao wengine mashaka matupu mara internet network inakata mara kwa mara ,

Wakati mwingine unajiunga bundle la GBs ukizani labda zimeisha kumbe zimo za kutosha isipokuwa tatizo liko Kwa TTCL wenyewe.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom