Ndugu zangu,
Tarehe kama hii mwaka jana nilitoa hoja Bungeni kuhusu Mkataba wa Buzwagi uliosainiwa kifisadi huko Uingereza.
Mengi yametokea katika Taifa letu toka Agosti mwaka 2007. Hebu tuangalie nyuma ili kuona tumefanikiwa nini katika vita dhidi ya ufisadi na pia wapi tumekosea na kuongeza nguvu zaidi ili Taifa letu liwe mahala pazuri pa kuishi. Kila mtu mwana JF, aseme anaona nini kimebadilika katika uendeshaji wa Taifa letu, katika vyama vya upinzani na katika chama tawala!
Vipi katika vyombo vya habari na Asasi zisizo za kiserikali?
Nawatakia kila la kheri, naenda ukumbini kuwajibika.............................. Lets look back and learn

Mabadiliko yapo. MAFISADI wakubwa kabisa angalau hawako SERIKALINI moja kwa moja ingawa MAKUWADI wao bado wamo. Kasi ya KUSAINI mikataba ya kuitafuna NCHI imepungua kidogo. JF imeendelea KUKOMAA na kutekeleza jukumu lake kikamilifu; Bunge linaendelea "kufufuka" kidogo;
Tarehe kama hii mwaka jana nilitoa hoja Bungeni kuhusu Mkataba wa Buzwagi uliosainiwa kifisadi huko Uingereza.
Mengi yametokea katika Taifa letu toka Agosti mwaka 2007. Hebu tuangalie nyuma ili kuona tumefanikiwa nini katika vita dhidi ya ufisadi na pia wapi tumekosea na kuongeza nguvu zaidi ili Taifa letu liwe mahala pazuri pa kuishi.
Bwana Zitto mbona hujajibu hoja ya msaada wa millioni 78 wa magari na pikipiki?
na uwiano wa kugawa ruzuku makao makuu na majimboni? mimi nilikuwa na mpango wa kujiunga na chama chenu lakini kwa hizo hoja nasita.
tunawaaminia kwa juhudi zenu hasa kwa hiii hoja uliyoileta lakini kwa nza safisha hali ya hewa bwana.
Nakutakia uwajibukaji mwema ukumbini wakati na mimi nawajibika hapa kijiweni kwangu.
...tuna bomu pale magogoni na hatuna hope kabisa...kajaa uswahili tuu na porojo huku marafiki zake wnamaliza nchi huku yeye kabakia kutuundia vitume vinavyomaliza pesa zetu zaidi,hasara tupu bora ifike muda aondoke tuu ila najua kuna siku akili itarudi na atajiona mjinga sana huyu JK maana kapewa dhamana ya nchi yeye anacheza tuu
Kandambili,Bwana Zitto mbona hujajibu hoja ya msaada wa millioni 78 wa magari na pikipiki?
na uwiano wa kugawa ruzuku makao makuu na majimboni? mimi nilikuwa na mpango wa kujiunga na chama chenu lakini kwa hizo hoja nasita.
tunawaaminia kwa juhudi zenu hasa kwa hiii hoja uliyoileta lakini kwa nza safisha hali ya hewa bwana.
Nakutakia uwajibukaji mwema ukumbini wakati na mimi nawajibika hapa kijiweni kwangu.
Kandambili,
Mhehsimiwa yuko hapa atakujibu tu,wanaiogopa hii maada kuhsu CHADEMa na wamemwachia Mnyika awasaidie kujibu
Ambaye hana Masters......