Tarehe/siku nzuri kwa mimba kuweza kutungwa

Duh! Thread ya tangu mwaka 2008. Ila nzuri.
 
Wakuu wana JF habari za weekend!

Naomba msaada tumuokoe jamaa yangu maana maji yamefika shingoni na demu wake ni mkali na hajui la kufanya kwa sasa.

Ni hivi: huyu jamaa alimpenda binti 1 mrembo tu hapa mtaani kwetu, binti alikubali na wakatoka out siku moja kula bata n.k. Lakini binti alimwambia kuwa ametoka kumaliza MP asubuhi ya siku hiyo but stil ana hofu ya kushika mimba. Yule msichana MP yake ni siku 5, so waka-do bila kinga siku hiyo coz men alijua hawezi pata mimba siku hiyo!

Ishu imeibuka kuwa demu anadai ana mimba na jamaa ndo mhusika! sasa jamaa haelewi how comes mimba ishike kwa siku hiyo ya 5 na ni asubuhi tu ndo amemaliza MP? Anachohisi ni kuwa demu ana-mbambikia hiyo mimba! Je afanye nini ili achomoke au kuhakikisha kama ni ya kwake?

Tusaidieni wataalamu plse!
 
Huwa hampendagi matokeo ya mambo mnayoyafanya ninyi wakaka. Sasa umefanya mambo bila kinga unatarajia nini? Hayo MP imeisha asubuhi au saa sita unayaamini je? Kama alikudanganya je? Kwa nn unakimbia kwenye kudanganywa zaidi badala ya kukaa na kuongea na huyo mwenzio ukaujua ukweli wa mambo, namaanisha kaa na huyo binti muulize vizuri iweje mimba ya kwako? Pengine ana majibu sahihi tu.
 
kama hayo maelezo ya jamaa ni ya kweli, then ana haki zote za kukataa hiyo mimba. Hamna ki2 kama hicho ktk biology.
 
Kiukweli kibiology kitu kama hicho hakipo.... Ila kinaweza kutokea kwa wale wanawake wenye FSH kwa wingi na LH pia! Hizi ni hormone zinazosababisha kutoka kwa yai kwenye Ovaries.. Sasa inaweza akawa amemaliza MP lakini yai jingine likatoka katika ovary nyingine.. Lakini huyo mwanamke si kwamba anamimba bali anahofu ya kupata mimba ndo mana amemwambia anahisi anamimba, sasa inaweza ikatokea akahisi mate machungu kumbe yametokana na ki2 kingine yeye akahisi ni MIMBA,sasa cha kufanya si kumfuata na kumwambia mimba aliyonayo ni ya m2 mwingne...FANY HIVI: Mwambie kuwa mimba kuipata wakat umetoka hedhi ni ki2 ambacho hakiwezekani halaf mwambie asubiri mpaka tarehe nyingne ya bleed aone kama hata bleed.. Mpe moyo kwamba ataingia period tu.....NA ki2 kimoja kinaweza tokea, anaweza akasubiri mpaka siku ya bleed lakini hata ikipita siku moja atakufuata na kuanza kukuuliza..mwambie asiwe na haraka ataingia 2, hiyo inawezwa sababishwa na hofu ndo mana ikapitiliza...ni hayo 2
 

ndo mambo ya kuchukua vitoto vya shule hayo; inaweza kuwa ni hofu tu ya binti, but in any case unapaswa uwe tayari kukubaliana na matokeo yoyote yanayotokana na matendo yako.
 
kama nilielewa soma la tarehe hatarishi, basi yawezekana kama binti ana less than 20days za kurudi MP.
 
Asikubali hapo hamna mimba wala nini.....saa zingine na sisi wanaume tuwe tunafikiria zaidi na sio kukubali tu ovyo ovyo kama hatujui kitu.....
 
One word of advice to your friend: DNA Test (actually thats two words, but you get the point)
 
Hiyo mimba yaweza kuwa ya huyo rafiki yako kwa sababu mbegu za kiume zinaweza kukaa kwa mwanamke kwa muda wa siku kuanzia 3 mpaka 5 zikiwa hai, na siku za kushika mimba zinahesabiwa kuanzia siku ya kwanza kuingia hedhi au ya MP; kwa maana hiyo siku 5 za MP jumlisha na 5 za mbegu ku-survive unapata siku 10 ambayo ina-posibility ya kutunga mimba. Lakini kwa upande mwingine yawezekana kuwa si yako kama kuna jamaa mwingine (wa hapo mtaani kwenu au la maanake huyo dada aweza kuwa nyama ya mtaa mzima) alimshughulikia siku ya 7 baada ya MP na mbegu zake kukaa mpaka siku ya 12 na kushika mimba.

Cha msingi akapime kwa daktari wakiwa wote wawili na kupata majibu wakiwa wote - tena waende kwa daktari wanayefahamiana naye. Kama ni kweli ni mjazito, jamaa alee hiyo mimba vizuri (ila arekodi gharama zote ata za kununua ubuyu), halafu mtoto akizaliwa ataangalia kama kuna reflection ya 'gene' yake au ya ukoo wao; kama hakuna reflection basi atasonga mbele kuangalia blood group; kama litakuwa sahihi na bado ana mashaka basi atasonga mbele kwenye 'gene machine'. Kama mtoto akiwa si wake basi mwanamke atarudisha gharama zote na kumpeleka mahakamani kwa kumchafulia jina.

Jamaa awe mvumilivu na mwenye busara ya hali ya juu. Pia siku nyingine atumie kondomu au kupima kwanza kabla ya kuchapa nyum nyum kwani UKIMWI hupo na unaua na kikombe cha Babu wala hakifui dafu!!!!!
 
Je, ni wiki ngapi za mama mjamzito (miezi mingapi) anatakiwa kuacha kuduu na mkewe aliye na hali hiyo?
 
Mko Sahihi LD na Riwa. Tangu nimeolewa natumia calender tu na sasa nina watoto wa3,wa kwanza wa kiume,wa pili wa kike na wa tatu wa kiume. Cha msingi ni kukumbuka kuhesabu kuanzia siku unayoanza na si unayomaliza hedhi. Thanks.
 
kWA KWELI hii thread imeniongezea ufahamu, haipitwi na wakati aisee! Big up Kungurumweupe kwa majibu mazuri, Hope nitayafanyia kazi muda si mrefu.
 
Wana JF kama unataka kujua siku zako za Bleed BONYA HAPA itaona mengi tu na kupanga uzazi

Kwa wanaume wakuu ingiza hizo details kutoka kwa mwezi wako au mkeo ili mpange mambo

asanteni
 
WanaJF mambo vp? Naombeni msaada kwenu.Mwenzi wangu huwa anaingia kwenye siku zake kati ya tarehe 8 au 10 lakini hadi leo tarehe 12 hajaona chochote na mara ya mwisho tuliduu tarehe 27.5.2011 vp kwa tarehe hizo ndo kitu kinaweza kuwa tayari kimeingia au vp? Yeye anasema anasikia tumbo linauma halafu linaacha naombeni ushauri wenu wa kiudaktari.Natanguliza shukrani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…