Tarehe za period kubadirika

Ziltan

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2011
Posts
2,672
Reaction score
6,880
Je ni kikwazo kwa kushika ujauzito au kawaida tu,
shemeji/wifi yenu ana hiyo hali.
Mf mwezi huu akiingia trh 20,
mwezi ujao atawahi kuingia kwenye trh 17.
Naombeni maelezo khs uhusiano wa trh hizo kuchange na kushika mimba.
Ahsanteni.
 
Wapi Mzizi mkavu,
tafadhali jaman msipite tu
 
Last edited by a moderator:
Angalia:

Mzunguko wa kawaida kwa mwanamke ni kati ya siku 21 hadi 35. Wastani ni siku 28.Assume mwezi huu(dec) ameingia tarehe moja..tunatarajia kwa mzunguko wa siku 28,ataingia tena kuanzia tarehe 28(dec). Mwezi huu una siku 31,kwa hiyo mwezi ujao(jan) ataingia kuanzia tarehe 25(sio 28!)..mwezi jao utakuwa na siku 31,so ataingia tena kuanzia trh 22 feb.Kwa hiyo ktk ipindi cha miezi mitatu tu kuna tofauti kubwa kutoka tarehe 28(dec) hadi 22(feb)!

Kwa hiyo ni kusema kwamba sio rahisi (kimahesabu) mwanamke kuwa na tarehe moja maalum ya kuona siku zake! Mara nyingi ataona siku zake siku 2-3 kabla ya tarehe aliyoingia mwezi uliopita. Na sababu kubwa ni hiyo ya mabadiliko ya siku za kalenda..tukumbuke miezi inatofautiana idadi ya siku,so hata mwanamke ni lazima siku zake zitakuwa zikienda zikibadilika.Hili limekuwa likiwasumbua sana akina mama. Wamekuwa wakitarajia kuona siku zao ktk tarehe moja maalum isiyobadilika..hili haliwezekani kutokana na sababu niliyokwishatoa.

Lakini pia tukumbuke kuwa binadamu sio kama kitabu..kuna mabadiliko miongoni mwetu kila siku.So sio ajabu mwanamke kukumbwa na mabadiliko hayo..hii ni pamoja na siku zao za mwezi.Mbali na factor hiyo ya kikalenda,pia mwanamke aweza kupata mabadiliko ktk siku zake kutokana na sababu za kimazingira kama vile mabadiliko ya hali ya hewa,hali yake kiafya,aina ya dawa na chakula anavyotumia,nk..nk..nk.

Kwa hiyo ndugu yangu,mimi nikutoe hofu tu kwamba shemeji/wifi yetu hali anayoiona ni kawaida.Cha msingi nyie endeleeni tu kufanya yenu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…